KATIKA
hali ya kawaida, tumezoea kuona watalii kutoka mataifa mbalimbali
duniani wakija nchini kuangalia vivutio vya utalii
vilivyopo.
Baadhi ya vivutio hivi
ni Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, majengo ya kale, mapango na nyumba za
kihistoria. Hata hivyo, kumeibuka aina mpya ya utalii, unaojulikana kama utalii
wa ngono, ambao unashamiri kwa kasi ukihusisha zaidi watalii wanawake wanaofuata
wanaume wa Kitanzania hasa vijana.
Uchunguzi uliofanywa na
Mwananchi Jumapili, unaonyesha kuwa utalii huo unaongezeka kwa kasi hasa katika
maeneo yenye vivutio vingi vya utalii ikiwamo Arusha, Kilimanjaro na
Zanzibar.
Imebainika kuwa katika
utalii huu, wanawake hasa watu wazima walio na umri kati ya miaka 60 hadi 80
kutoka nchi mbalimbali, wamekuwa wakiingia nchini kwa lengo la kutafuta vijana
wa kiume wa kustarehe nao.
Uchunguzi huo
unaonyesha kuwa wanawake ambao hawana vigezo vya uzuri vinavyopendwa na wanaume
huko kwao, ikiwamo wembamba na urefu, husafiri kuja Tanzania kutafuta mwanamume
atakayestarehe naye kingono. Hali hiyo inawakumba zaidi wanawake wanene, ambao
kwa Ulaya hukosa wapenzi, hivyo kulazimika kusafiri kuja Afrika Tanzania ikiwamo
kutafuta mwenza wa kustarehe nao.
Uchunguzi uliofanywa
na gazeti hili umebaini kuwa, utalii huu umeshamiri nchini, ambapo vijana wa
Kitanzania wanaufahamu na kukiri kuwa umewanufaisha na baadhi yao kuwasaidia
kupata tiketi za kwenda kuishi Ulaya. Katika Visiwa vya Zanzibar utalii huo
unafanyika zaidi katika fukwe za Nungwi, Kiwengwa, Paje, Kendwa, Jambiani na
maeneo mengine yaliyopo pembezoni mwa bahari.
Katika fukwe hizo
vijana maalumu kwa kazi hiyo, wana kauli mbiu yao inayosema:“apewe mpaka
apagawe, atoe tiketi.”
Kwa kauli mbiu hiyo
vijana hao wanamaanisha kuwa, kwa kila mwanamke watakayekutana naye, watatumia
kila mbinu ili kumfurahisha hadi awasafirishe au kwenda naye Ulaya. Abdulla Ali
Haji (Sio jina halisi) ni miongoni wa vijana wanaojihusisha na aina hiyo ya
utalii, akiishi visiwani humo ambapo anaeleza kuwa shughuli yake kubwa ni
kuzunguka katika fukwe mbalimbali akiwinda wanawake wa kizungu wanaotaka
kustarehe.
|
Post a Comment