Mwakilishi wa Mbunge wa Temeke, Thabit Mussa akikata
utepe wakati wa uzinduzi wa jengo la benki ya Advanc, Temeke jijini Dar es
Salaam jana. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Peter Moelders na
kulia ni Kaimu Meneja wa benki hiyo, Boniface Mhali na diwani wa Temeke, Hamisi
Msombo. (Picha na Habari Mseto Blog)
Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Benki ya Advanc, Peter Moelders akisakata muziki wa asili na msanii wa kundi la
Wanne Star, wakati wa uzinduzi wa benki hiyo, Temeke jijini Dar es
Salaam.
Wasanii wa kundi la Wanne
Star na kundi lake akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa tawi la benki mpya ya
Advanc, Temeke jijini Dar es Salam jana
DAR ES SALAAM,
Tanzania
BENKI ya Advanc imetakiwa
kuonyesha tofauti yao na benki zingine kwa kutoa riba nafuu na masharti
yanayowezekana kwa wakopaji ili kulisaidia Taifa kiuchumi kupitia wajasiriamali
wadogo.
Akizungumza wakati wa
uzinduzi wa tawi la benki hiyo wilayani Temeke jana, mwakilishi wa mbunge wa
Temeke, Thabit Massa alisema ingawa kuna benki nyingi nchini lakini riba na
masharti magumu yanafisha ari ya watu kukopa.
Mwakilishi huyo wa mbunge
alisema kufunguliwa kwa tawi hilo kunafanya Temeke kuwa na matawi saba sasa ya
benki lakini bado hakujawa na mafanikio tarajiwa na mbaya zaidi baadhi ya benki
hizo hazina huduma nzuri kwa wateja.
“Lugha nzuri hakuna na hata
mikopo imekuwa ikitolewa kwa kujuana baina ya wakopaji na watendaji wa baadhi ya
benki jambo ambalo sio jema na linashusha imani ya wateja kwa benki” alisema na
kuongeza kuwa anatarajia mabadiliko.
Alisema beni hiyo inatakiwa
ije na mambo tofauti ili kuleta tija kwa wakazi wa eneo hilo tofauti na ilivyo
sasa na awali Mtendaji mkuu wa benki hiyo, Moelders alisema wamekuja ulata
mapinduzi makubwa katika uduma za kibenki nchini.
“Benki yetu walengwa wake na
wananchi wa kawaida na wale waliopo vijijini na kabla ya mwisho wa mwaka huu
itafungua matawi mawili Jijini Mwanza na mwakani watazindua matawi mengine ya
idadi hiyo Jiji la Mbeya
Imechotwa: Habari Mseto


Post a Comment