Mashabiki wa Bar ya East
Africa wakishangilia mara baada ya kutangazwa washindi wakati wa shindano la
Safari Nyama Choma lililofanyika katika Viwanja vya CCM Mkoa Mwishoni mwa
wiki.
Na Mwandishi Wetu,
Moshi
EAST AFRICA BAR, wametwaa
ubingwa wa mashindano ya Nyama Choma Mkoa wa Moshi, baada ya kuzigaragaza baa
nne zilizotinga fainali ya mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) kupitia bia ya Safari Lager.
Kwa kutwaa ubingwa huo katika
fainali zilizofanyika juzi Jumapili kwenye Viwanja vya CCM Mkoa , baa hiyo
ilizawadiwa fedha taslim Sh milioni moja pamoja na cheti.
Waliokuwa mabingwa watetezi wa
mashindano hayo mkoani hapa, Makanyaga Bar, walishika nafasi ya pili na kuondoka
na kitita cha Sh 800,000 na cheti, wakati White Star Pub walishika nafasi ya
tatu na kupata zawadi ya Sh 600,000 na cheti.
Walioibuka na nafasi ya nne ni
baa ya Forest Bar iliyozawadiwa Sh 400,000 na cheti, wakati baa ya Lamina
ilishika nafasi ya tano na kuzawadiwa Sh 200,000 na cheti.
Akizungumza kabla ya kumtangaza
mshindi, Jaji Mkuu wa fainali hizo, Douglas Sakibu, alisema kuwa walitoa mafunzo
kwa baa zote hizo juu ya mambo wanayopaswa kuzingatia katika uchomaji
nyama.
Alivitaja vigezo walivyotumia
kupata mshindi kuwa ni usafi wa mchomaji, vifaa na mazingira, maandalizi ya
nyama kuanzia uchaguzi, uhifadhi wake na wa vifaa.
Vingine ni uchomaji na upangaji
nyama, ladha na ulaini wake, mazingira ya eneo, mtiririko wa maji na uhifadhi wa
taka.
Akizungumza kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo,
alisema kuwa ni fahari kubwa kwa TBL na bia ya Safari Lager kwa ujumla
kufanikisha shindano hilo mkoani ambao ndio mkoa wa mwisho.
“Tulianza kwa kuwataka watu
wapige kura kupendekeza baa zinazofaa kuingia katika shindano la nyama choma kwa
mkoa huu wa Moshi tukapata baa hizi tano zilizoingia fainali ambapo leo
tutampata mshindi.
“Tunajua watu huwa wanakwenda
katika baa na kula nyama hivyo tukaona ni vema tuanzishe mashindano haya ili
walaji nyama choma wapate nyama bora,” alisema.
Alisema kuwa bia ya Safari Lager
ina miaka takriani 36 na bado imeendelea kuwapo hadi sasa ambapo ndio inayoongoza kwa
mauzo.
Kwa upande wake, mgeni rasmi
ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Dr.Ibrahim Msengi, aliisifu TBL
kupitia Safari Lager kwa kuandaa mashindano hayo, akisema kuwa serikali
inatambua mchango wa kampuni hiyo katika kujenga uchumi wa Taifa kupitia tukio
hilo na mengineyo kama mashindano ya Pool Safari Lager, Safari Wezesha na hata
udhamini wao katika michezo mbalimbali kama soka na mingineyo.
“Mashindano haya ni mazuri kwani
yanawajengea wateja wa nyama mazingira mazuri na salama katika kutoa huduma hii
ya nyama choma,” alisema.
Alizitaka baa ambazo
hazikufika fainali, kutokata tamaa na badala yake kujipanga kwa ajili ya
mashindano ya mwakani, kwa kurekebisha yale waliyokosea mwaka huu


Post a Comment