|
NDUDU WA SAMSON DANIEL
ALIYOWATEKETEZA KWA MOTO 2010
*************
Mahakama kuu Kanda ya Mbeya imemhukumu kutumikia kifungo
cha miaka 35 Samsoni Daniel Mwang’ombe baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila
kukusudia ndugu wa familia moja wapatao saba.
Akisoma mashtaka mbele ya jaji wa mahakama hiyo Samwel
Karua, Mwendesha mashtaka wa Serikali Rhoda Ngole alisema mtuhumiwa huyo
alitenda kosa hilo Juni 21, 2010 kinyume cha kifungu cha 195 (16) kilichofanyiwa
marekebisho Mwaka 2002.
Ngole aliiambia Mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda
kosa hilo mwaka huo majira ya 2:00 hadi saa 2:30 usiku ambapo alifika nyumbani
kwa baba yake akiwa na sigala mkononi huku akiivuta na baadaye kuidondosha
sigala hiyo iliyosababisha moto kuwasha nyumba.
Aliwataja walioathirika na moto uliokuwa umewashwa
kutokana na sigala aliyokuwa ameidondosha mtuhumiwa kuwa ni Daniel Mwang’ombe,
Anitha Richard, Salome Mwang’ombe,Jane Samson, Diana Samson, Maria George na
Cloud Samson.
Kutokana na kosa hilo mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na
kwamba aliua bila kukusudia ambapo alikiri kuwa akiwa anavuta sigala alidondosha
kipande hicho ambacho kilikuwa bado kinawaka moto.
Aidha Mwendesha huyo aliiambia mahakama hiyo kuwa pamoja
na mtuhumiwa kukiri kusababisha vifo bila kukusudia mahakama impe adhabu kali
kwa mujibu wa sheria.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo Wakili wa upande wa
utetezi Sambwee Shitambala alisema Mahakama inatakiwa kumwonea huruma na
kumpunguzia adhabu mshtakiwa kutokana nay eye kuwa miongoni mwa
wafiwa.
Alisema mshtakiwa ameondokewa na wazazi, watoto na mke
katika ajali hiyo ambapo hakuhudhuria mazishi yao pia amekaa muda mrefu akiwa
mahabusu ambapo amekaa kwa miaka mitatu na kuongeza kuwa mtuhumiwa ni kijana
ambaye ni nguvu kazi ya taifa hivyo hastahili kufungwa.
Hata hivyo kutokana na utetezi huo Jaji Karua alisema
kutokana na hali iliyojitokeza mtuhumiwa atatumikia kifungo cha miaka mitano kwa
kila tukio ambalo ni kusababisha vifo saba hivyo jumla atatumikia miaka
35
Na
Venance Matinya, Mbeya.
|
on Saturday, March 16, 2013
Post a Comment