Ni Mhitimu wa Chuo
Kikuu Cha Sokoine Morogoro (SUA ), Mkaazi wa Njombe! Zawadi Nono Ya
Fedha Taslimu, Shilingi Laki Tano ( Tsh.500,000/=) Za Kitanzania,
kutolewa kwa mtu atakaye fanikishwa kukamatwa kwa tapeli hili la
mtandaoni.
Hatimaye yule tapeli
sugu wa mtandaoni aliyekuwa akiwatapeli wananchi mbalimbali kwa jina la
RafikiElimu akiwahadaa kuwapatia ajira ajulikana .
INAPOTOKA : Mnamo siku ya tarehe 11 Machi
2013, tuliripoti kupitia blogu yetu na katika blogu mbalimbali nchini
kuhusu kuwepo kwa mtu anaye watapeli wananchi fedha kwa kutumia
jina la taasisi yetu. Tapeli huyu asiye na hata chembe ya
huruma kwa masikini wenzake, aliweka tangazo katika mtandao wa
Zoom Tanzania, mnamo mwanzoni mwa mwezi February 2013 akitangaza nafasi
za kazi z a kuvolunteer katika mikoa mbali mbali ya Tanzania bara.
Baada ya watu kutuma maombi yao, tapeli huyo
aliyekuwa akijitambulisha kwa jina bandia
la EMMANUEL ALBERT na kwamba yeye ni HR wa RafikiElimu, aliwaambia
kuwa wamepata nafasi, na kuwatumia fomu za kujaza kisha kuwataka
wamtumie
shilingi elfu Tano ( Tshs. 5,000/=) za
kitanzania kwa mpesa kwenda namba 0763906931 ( AMBAYO MBAYA
ZAIDI AMEISAJILI KWA JINA LA RAFIKIELIMU ).. Baada ya kumtumia pesa ,
tapeli huyo aliwatumia barua na kuwaagiza kuripoti kazini katika taasisi
mbalimbali, huku mmoja kati yao akimuagiza aje kuripoti katika ofisi
zetu.
Tulibaini juu ya uwepo wa utapeli huu
mara baada ya kutembelewa na mmoja kati ya wahanga wa utapeli huo.
Dada huyo aliye jitambulisha kwa jina la HAWA MUSSA ambaye ni Muhitimu
wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ( 2012 ) aliripoti katika ofisi zetu siku
ya tarehe 11 Machi 2013 saa nne kamili
asubuhi na kuomba kumuona HR . Baada ya
kufanya naye mazungumzo ndipo tulipo baini kuwepo kwa utapeli unao
fanyika kwa jina la taasisi yetu. Haraka haraka tukaenda
kuripoti uhalifu huu kwenye kituo kidogo cha polisi cha Chuo Kikuu Cha
Dar Es salaam, na kukabidhiwa RB namba UD/RB/849/2013 WIZI
KWA NJIA YA
MTANDAO.
source michuzi
matukio

Post a Comment