Balozi
wa Tanzania Nchini China, Philip Marmo akizungumza baada ya
kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake,
nyumbani kwake, kwenye Ubalozi wa Tanzania mjini Beijing, China, baada
ya kuwasili leo Machi 17, 2013, akitokea jimbo la Sichuan. Kinana na
ujumbe wa viongozi 14 wa CCM wapo nchini China kwa ziara ya siku kumi ya
mafunzo, kwa mwaliko wa Chama CHa Kikomunisti cha China. Kushoto ni
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
"KARIBU
BEIJING", Balozi wa Tanzania nchini China, Philip Marmo (kulia)
akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kwenye Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Beijing, China, baada ya Kinana na ujumbe wake
kuwasili akitokea jimbo la Sichuani, leo Machi 17, 2013. Kinana na
ujumbe wa viongozi 14 wa CCM wapo nchini china kwa ziara ya siku kumi ya
mafunzo, kwa mwaliko wa Chama CHa Kikomunisti cha China.
Baadhi
ya Watanzania waliopo jijini Beijing, China wakichangamkia kupigapicha
na Katibu wa NEC, Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose
Migiro (Katikati) nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini China.
Baadhi
ya Watanzania wanaoishi Beijing, wakilaki Kinana na msafara wake,
nyumbani kwa Balozi Marmo, Beijing China, leo Machi 17, 2013. Kulia ni
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Beijing, Daninga
.Daniel. Picha na Bashir Nkoromo
Post a Comment