MwananchiJohannesburg.
Mkurugen-zi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba amezung-umzia ugonjwa wake
ambao ulisababisha kutojitambua kwa siku 42 na kwamba sasa anaendelea
vizuri.
Kwa sasa Manumba ambaye
amelazwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu, anaendelea vizuri na sasa anafanya
mazoezi mepesi ya kusimama na kutembea kama sehemu ya matibabu
yake.
“Kwa sasa ninashukuru
naendelea vizuri, nina-washukuru madaktari wa hapa ambao wamejitahidi maana ni
kama watu wal-ishakata tamaa kwamba siwezi kupona,” alisema Manumba
alipozungumza na Mwananchi katika Hos-pitali ya Millpark alikolazwa jijini
Johannesburg.
Alisema tatizo kubwa
lili-lokuwa likimkabili ni ugon-jwa wa malaria kwani ali-popimwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili alikutwa na wadudu wa ugonjwa huo
500.
Manumba anasema ni kwa
mkono wa Mungu amepa-ta nafuu kubwa baada ya juhudi kubwa za madaktari katika
kupigania uhai wake.
Alipelekwa Afrika Kusini
Januari 23, mwaka huu baa-da ya kupata nafuu kidogo.
Alisema anawashukuru
madaktari wote walio-hangaika usiku na mchana katika hospitali alizolazwa
kuanzia Muhimbili na Aga Khan, jijini Dar es Salaam, kabla ya kusafirishwa kwa
ndege maalumu hadi Johan-nesburg, Afrika Kusini.
Kadhalika alilimshukuru
Rais Jakaya Kikwete kwam-ba ndiye alisaidia kuhara-kishwa kwa mchakato wa
kuhamishiwa jijini hapa kwa ajili ya matibabu zaidi ambayo yamemrejeshea uzima
ambao tayari ulikuwa kama umepotea. “
Kwa kweli sasa kama
mnavyoniona sijambo sana. Nimeanza kufanya mazoezi. Sijambo kwa kweli inga-wa
bado niko hospitalini naendelea na matibabu,” alisema
Manumba.
Wakati huohuo,
Mwe-nyekiti wa Jukwaa la Waha-riri Tanzania (TEF), Absa-lom Kibanda,
amezungum-zia tukio la kuvamiwa kwake huku akiweka bayana kuwa, watesi wake
walikusudia kumtoa uhai.
“Kwa muda mrefu
nili-kuwa nimedokezwa na rafiki yangu mmoja kuwa ninapokwenda nyumbani niwe
mwangalifu kuanga-lia nani hasa yuko nyuma yangu usiku, lakini kwa siku ile
sikuona kama kuna watu walikuwa wakinifuatilia,” alisema katika mahojiano na
gazeti Mwananchi.
Post a Comment