Baada ya kikao cha ndani
kati ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji Wilaya ya Tarime na madiwani, kubaini
udhaifu wa kiuongozi ulioruhusu kuzuka kwa makundi yaliyokuwa yakidhoofisha
utendaji kazi na uhai wa chama wilayani hapa, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,
Freeman Mbowe amevunja uongozi wa wilaya hiyo (kwa maana ya Kamati ya
Utendaji).
Uamuzi huo uliofanyika
leo mchana, ulipokelewa kwa mikono miwili na wajumbe wa kikao
hicho.
Baada ya kikao hicho cha
Kamati ya Utendaji na madiwani wa CHADEMA Wilaya ya Tarime, Mwenyekiti Mbowe
alikutana na wanachama na wadau wa chama wa Tarime, kwenye kikao cha ndani,
ambapo kwa kauli moja waliupokea kwa furaha uamuzi huo wa kuvunjwa kwa uongozi
huo, huku wakiomba nafasi hizo za uongozi zijazwe mapema kwa ajili ya kuendelea
kukiimarisha chama.
Uongozi wa chama katika
ngazi za kata hadi misingi utaendelea kufanya kazi kama
kawaida.
Kwa hatua hiyo, uchaguzi
wa kupata uongozi wa Kamati ya Utendaji ya muda, utafanyika ndani ya mwezi mmoja
ukisimamiwa na ngazi ya juu
Mwenyekiti Mbowe
amewataka watu wa Tarime kutopoteza ari yao ya dhati katika kukisimamia na
kukipigania CHADEMA katika kuendesha mapambano ya ukombozi wa pili wa nchi,
ambayo ilikuwa ni mfano wa kuigwa wa wanaChadema nchi nzima, kiasi cha watu
kusalimiana..."mambo...kama
Tarime..."
Post a Comment