Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimemtupia lawama nzito Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar
Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuanza kwenda kinyume na makubaliano yaliounda
Serikali ya Umoaja wa Kitaifa mwaka 2009.
Akihutubia mamia ya wanachama na mashabiki wa CCM waliohuidhuria mkutano wa
hadhara uloiofanyika Jumba la Vigae huko Jang’ombe mjini Ungujajana(3.3.13),
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar, Vuai Ali Vuai amesema Maalim Seif ameanza
kufanya vikao vya siri vinavyotishia kuvuruga amani na umoja wa kitaifa Visiwani
humu.
Vuia ambaye ni
kati ya wajumbe waasisi walioshiriki katika mchakato wa mazungumzo ya
upatanishi wa kisiasa Zanazibar, amesema kama angeliijua mapema dhamira ya
Maalim Seif katika mazungumzo ya kundwa kwa Serikali iliyopo, angekuwa radhi
kujitoa na kutokuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya
muafaka.
Amesema kwamba
hivi karibuni kiongozi huyo ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF, ameitisha kikao maalum
cha vijana wa chama chake na kusema, ikiwa chama chake kitawaamrisha vijana,
nchi haitatawalika na ikibidi litote tugawane mbao.
Aidha Naibu huyo
Katibu Mkuu amesema msingi wa mazungumzo ya vyama vya CCM na CUF katika awamu
zote za kusaka maridhiano ya kisiasa yalihimiza kujengeka kwa hali ya amani,
utulivu na mshikamano wa kitaifa.
Vuai ameiita
kauli hiyo ni ya kichochezi na kwamba haikubaliki mbele ya jamii na kuwatolea
wito viongozi wa kisiasa na kiserikali kuchunga ndimi zao ili kuyaenzi mazingira
yalioleta maridhiano ya kisiasa.
Amesema Maalim
Seif kama anataka litote ili wagawane mbao ni heri akachukua mapema ubao wake na
kuelekea Mtwambwe na kwamba CCM haiko tayari kuona kuona amani ya Zanzibar
ikichezewa kwa maslahi binafsi.
Naibu
huyo Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar amesema miongoni mwa mambo waliokubaliana
katika mchakato wa mazungumzo ya kusaka upatanisha , yamewaaasa wanasiasa
kutotoa kauli na matamshi makali yanayoweza kuiparaganya tena
Zanzibar.
Amesema kwa muda
wa mwaka mmoja CCM kimekuwa hakifanyi mikutano ya hadhara kwa kuheshimu
makubaliano hayo lakini CUF viongozi wake wamekuwa wakiendesha mikutano yenye
kejeli na vitisho yanayoweza kuirudisha nyuma Zanaibar mahali
ilikotoka.
Akizungumzia madai ya kuwepo kwa utata wa Muungano,
Vuai amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni halali na kuwataka wanasiasa
wanaopotosha jambo hilo kutafakari kwa kina faida zitokanazo na kuwepo kwake
pia athari ikiwa Muungano huo utavunjika.
SOURCE::WAVUTI::
Post a Comment