Katibu wa CCM itikadi na Uenezi Nape
Nnauye
--
Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa
ya kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na
Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ndugu Absalom Kibanda usiku wa kuamkia
Jumatano Machi 6, 2013.
Chama Cha Mapinduzi kinalaani kwa nguvu zote kilichotokea
kwa Absalom Kibanda, kwani ni unyama usiokubalika hata kidogo, unafaa kulaaniwa
na Watanzania wote.
CCM
tunaitaka Serikali kuhakikisha inawapata waliofanya unyama huo na kuwafikisha
mbele ya vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake, na kukomesha matukio
ya namna hiyo.
Aidha, Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa Uongozi wa
Jukwaa la Wahariri, Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006, familia ya Ndugu
Kibanda, wanahabari na wadau wote wa habari nchini, na tunamwombea kwa Mwenyezi
Mungu apone haraka na kurejea katika kazi zake za Ujenzi wa
Taifa.
Imetolewa na:
Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA
TAIFA,
ITIKADI NA UEENEZI
08/03/2013
Post a Comment