Watoto wa
watawala wa kwanza wa Nchi ya Kenya, Rais Jomo Kenyatta na Makamu wake wa Kwanza
wa Rais Jaramogi Odinga Odinga wanazidi kuchuana vikali kuwania kiti cha Urais
Kenya huku Kenyatta akiwa mbele kwa tofauti ya kura zaidi ya
1,036,834.
Matokeo ya
Uchaguzi nchini Kenya hadi kufikia Usiku wa
Machi nane saa 3:45
yalionesha kuwa Uhuru Kenyata alikuwa mbele kwa kura 5, 824,901
dhidi ya kura 4,788,067 za Mgombea wa ODM, Raila
Odinga.
Hadi kufikia
muda huo ni kura
11,359,686
ndio zilikuwa zimekwisha hesabiwa kutoka katika
majimbo 264 kati ya majimbo 291 ya Uchaguzi.
Aidha katika
kura hizo kura
100,567
zimeharibika hivyo kufanya kura halali hadi sasa
kufikia
11,251.
Katika
kinyang’anyiro hicho Wycliffe Musalia
Mudavadi anashika nafasi ya tatu akiwa
amejikusanyia kura
431,056
a nafasi ya nne ikienda kwa Peter
Kenneth mwenye kura
66,999.
Mgombea wa
Alliance for Real Change,Mohamud Abduba
Dida anashika nafasi ya tano akiwa na kura
51,093
akifuatiwa na Mwana mama Martha Karua wa
National Rainbow Coalition mwenye kura
40,309 hadi
sasa.
Nafasi ya
saba katika wagombea hao Urais inakwenda kwa James
ole Kiyiapi wa Chama cha
Restore and Build Kenya ambaye ana kura 36,
317 huku nafasi ya ya nane na mwisho ikishikwa
na Paul Kibugi Muite wa chama cha
Safina.
WAJUE WAGOMBEA URAIS NCHINI KENYA
2013
Raila Amollo
Odinga
Waziri Mkuu Raila
Amollo Odinga alizaliwa Januari 7, 1945 huko Maseno, Nyanza, mtoto wa Makamu wa
Rais wa kwanza Jaramogi Oginga Odinga. Anagombea kupitia kupitia ushirika wa
CORD na Makamu Rais Kalonzo Musyoka akiwa mgombea mwenza wake. Odinga ametilia
mkazo maswala ya vijana katika kampeni yake, akiahidi kuwasaidia kuwapatia kazi
zaidi na elimu. Odinga alijihusisha katika siasa za upinzani kwa miaka mingi
kabla ya kuteuliwa Waziri Mkuu katika muafaka uliofuatia ghasia za uchaguzi wa
mwaka 2007.
Uhuru Muigai Kenyatta
Uhuru Muigai Kenyatta
alizaliwa Octoba 1961. Baba yake ni rais wa kwanza wa Kenya Jomo Kenyatta,
ambaye aliongoza Kenya kutoka 1964 mpaka 1978. Anawania urais kama mgombea wa
Jubilee Alliance, ulioundwa kwa ushirikiano wa chama cha The National Alliance
cha Kenyatta na United Republican cha William Ruto. Katika ushirika wao,
Kenyatta anasema anasimamia Kenya iliyoungana chini ya “ndoto moja ya kujenga
Kenya bora”. Aliwania urais 2007, lakini baadaye akamwunga mkono Rais Mwai
Kibaki. Kibaki alimchagua Kenyatta kama waziri wa serikali za mitaa Januari
2008 kabla ya kuwa naibu makamu waziri mkuu na waziri fedha mwaka 2008 kama
sehemu ya mapatano ya serikali ya ushirika kumliza ghasia za baada ya uchaguzi
za mwaka 2007.
Mohamud Abduba Dida
Mohamud Abduba Dida
alizaliwa katika wilaya ya Wajir mwaka 1975. Mwalimu wa zamani, Dida anagombania
urais kupitia Alliance for Real Change. Mgombea wake mwenza ni Joshua Odongo
Onono, pia mwalimu wa zamani. Dida, mwanasiasa mpya, ameahidi kutilia mkazo
masikini kama rais. Anasema elimu ni budi iwe bure kwa Wakenya. Alisifiwa kwa
kufanya vizuri sana katika midahalo yote miwili ya urais iliyofanyika kwa mara
ya kwanza Kenya katika matayarisho ya uchaguzi.
Martha Karua
Martha Karua, mgombea
pekee mwanamke katika uchaguzi huu, alizaliwa Septemba 1957 huko Kirinyaga,
Central Province. Karua, mbunge wa Gichugu, anagombania kupitia ushirika wa
National Rainbow Coalition akifuatana na mbunge wa zamani wa bunge la Afrika
Mashariki, Augustine Lotodo. Karua ameahidi kuwakilisha Kenya iliyoungana na
maswala ya mageuzi ya uchumi nay a kijamii, ikiwa ni pamoja na afya kwa wote.
Anasema atatumia asilimia 10 ya bajeti ya Kenya kuboresha uzalishaji katika
kilimo, kuongeza uzalishaji nishati na kuhakikisha asilimia 50 ya nyumba za
Kenya zinapata huduma wa mtandao katika muda wa miaka
mitano.
Peter Kenneth
Peter Kenneth
Peter Kenneth
alizaliwa Novemba 1965 Bahati, Nairobi. Ni mbunge ambaye anajulikana kwa uhodari
katika maswala ya fedha na benki. Anawania urais kupitia chama cha Kenya
National Congress, na mgombea mwenza wake ni Ronald Osumba, meneja wa zamani
katika kampuni ya simu ya Safaricom. Kama mgombea, Kenneth ametilia mkazo
kupunguza ukosefu wa kazi na kukosekana kwa chakula. Kutoka mwaka 2003 mpaka
2005, alikuwa waziri mdogo katika wizara ya Maendeleo na Masoko, na baadaye kama
waziri mdogo katika Wizara ya Fedha mpaka 2007. Tangu mwaka 2008, amekuwa waziri
mdogo katika Wizara ya Mipango, Maendeleo ya Taifa na Dira ya
2030.
James ole Kiyiapi
James ole Kiyiapi
alizaliwa Mei 1961 huko Osupuko, Rift Valley Province. Alifanya kazi kama
katibu mkuu katika wizara mbali mbali kabla ya kujiuzulu mwaka 2012, anafuatana
na mfanyabiashara Winnie Kaburu kama mgombea mwenza chini ya chama cha Restore
and Build Kenya. Kiyiapi anagombania kwa nguvu ya swala la kuondoa ukabila
katika siasa za Kenya. Anasema kipaumbele chake cha kwanza kama akichaguliwa
itakuwa kutilia mkazo vijana na ukosefu wa kazi. Anasema serikali yake
itaanzisha mpango wa kupata ufumbuzi wa matatizo ya ardhi kwa uangalifu na
uwazi, na kuboresha uzalishaji kilimo nchini.
Wycliffe Musalia Mudavadi
Naibu Waziri Mkuu
Wycliffe Musalia Mudavadi alizaliwa September 1960 huko Sabatia, Western
Province. Anagombania chini ya chama cha United Democratic Forum Party katika
ushirika wa Amani alliance, na Jeremiah Kioni, mbunge kutoka Ndaragwa. Mudavadi
ameahidi kuleta ukuaji wa kweli wa uchumi Kenya kwa kutilia mkazi utawala bora
na kupunguza umasikini. Mudavadi alikuwa mbunge mwaka 1989, alipochaguliwa
bilwa kupingwa kuchukua nafasi ya marehemu baba yake Moses Mudavadi, katika
jimbo la Sabatia.
Paul Kibugi Muite
Paul Kibugi Muite
alizaliwa Aprili 1945. Ni mbunge wa zamani kutoka jimbo la Kabete ambaye pia ni
mmoja wa waanzilisha wa chama cha Safina. Anashirikiana na Shem Ochuodho, waziri
wa zamani wa nishati na mbunge wa Rangwe. Muite anasema akiwa rais
atashughulikia swala la ukosefu wa kazi na kuboresha hali ya utendaji kazi kwa
kuongeza mishahara nja kutekeleza sheria za kazi ambazo zitaweka kiwango cha
masaa ya kazi kuwa manane pekee kwa siku. Anasema anaamini umoja wa wananchi wa
Kenya, bila kujali ukabia, na atashughulika kuboresha hali ya watu wote. Muite,
ambaye ni mwanasheria wa haki za binadamu, alikuwa miongoni mwa viongozi
mashuhuri walioshinikiza kumaliza kwa siasa za chama kimoja katika miaka ya
1990.
Credits: Father Kidevu
Post a Comment