Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mhariri Mtendaji wa
Habari Corporation Absalom Kibanda aliyelazwa katika hospitali ya Mill Park
iliyopo mji wa Johannesburg, Afrika ya Kusini leo jioni.Kulia ni Katibu mkuu wa
CCM Abdulrahman Kinana.Bwana Kibanda alipelekwa Afrika ya kusini kwa matibabu
zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana juzi usiku.Rais Kikwete
yupo Afrika ya Kusini kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa
mstari wa Mbele katika mapambano dhidi ya Ukoloni na ubaguzi wa Rangi.Mkutano
huo umeandaliwa na Chama cha African National Congress(ANC).
Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete katika ukumbi wa Freeedom Park mjini Pretoria Afrika ya Kusini
kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyioshiriki katika harakati za
ukombozi Kusini Mwa Afrika.
Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini(Katikati) akiongea na
waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Viongozi wa vyama
vilivyokuwa mstari mbele katika harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika leo
mchana.Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa FreedomPark,Jijini Pretoria
Afrika ya Kusini. Kushoto ni Rais Jakaya Kikwete mbaye pia ni Mwenyekiti wa CCM
na kulia ni Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye ni kiongozi wa ZANU PF.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM akiwa
katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini
ambaye pia ni kiongozi wa ANC(Watatu kushoto),Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe
ambaye pia ni kiongozi wa ZANU PF(Wapili kushoto) pamoja na Waziri Mkuu wa
Namibia aliyeiwakilisha SWAPO, muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wao
uliofanyika katika ukumbi wa Freedom Park,jijini Pretoria nchini Afrika ya
Kusini kwa mwaliko wa chama tawala cha Afrika ya Kusini ANC.(picha na Freddy
Maro).
Post a Comment