Watu
watatu wamefikishwa mahakamani katika mikoa ya Kilimanjaro, Dodoma na Mkoa mpya
wa Simiyu kwa tuhuma za kutumia lugha za matusi na uchochezi dhidi ya Spika wa
Bunge la Jamhuri yak Muungano wa Tanzania.
Mkurugenzi wa
idara ya habari maelezo ASSAH MWAMBENE ameiambia Clouds Fm kwamba watu wawili
walikamatwa kwa tuhuma za kumtumia ujumbe mfupi wa maneno wenye lugha za matusi
na mmoja alikamatwa na DVD yenye picha za kuhamasisha lugha za matusi kwa spika
wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ANNE MAKINDA.
Mapema
mwezi uliopita spika MAKINDA alipokea ujumbe mara 400 kwa njia ya simu ya
mkononi, pamoja na kupokea simu zote zikiwa na lugha yak matusi, kufuatia namba
ya spika kutangazwa hadharani katika mkutano wa chama kimoja cha siasa hapa
nchini.
Post a Comment