Dar es Salaam.
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Aprili 18, mwaka huu
inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (55) na wenzake
49.
Mbali na
kupangwa kwa tarehe ya hukumu hiyo, Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa jana
aliutaka upande wa mashtaka na utetezi kuwasilisha hoja zao kama
washtakiwa hao watakuwa na hatia ama la, Aprili 3, mwaka huu.
Juzi
wakati Sheikh Ponda akijitetea aliieleza mahakama hiyo, kuwa yeye hana
nyaraka za umiliki wa Kiwanja cha Malkazi Chang’ombe bali historia ya
eneo hilo inawafanya wao kuwa wamiliki.endelea kupitia audifacejackson blogspot,,
Sheikh
Ponda na wenzake hao 49, wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kuingia
kwa jinai, kuvamia ardhi inayomilikiwa na Kampuni ya Agritanza Ltd kwa
nia ya kujimilikisha isivyo halali, wizi wa mali yenye thamani ya Sh
59.6 milioni na uchochezi.
Akijitetea
dhidi ya mashtaka hayo, Sheikh Ponda, akiongozwa na wakili wake, Juma
Nassoro, alidai kuwa awali kiwanja hicho kilikuwa kinamilikiwa na
Taasisi ya Jumuiya ya Kiislamu ya East African Muslim Welfare Society
(EAMWS) ambayo ilivunjwa na Serikali mwaka 1958 na Serikali kuunda
chombo kingine kilichosajiliwa kama Bakwata.
Alidai
kuwa Bakwata iliundwa ili kusimamia shughuli zilizokuwa zikiendeshwa na
Taasisi ya Jumuiya ya Kiislamu ya East African Muslim Welfare Society na
siyo mali kama majengo, viwanja na hata shule.
“Tulitumia
njia ya mazungumzo ya kidiplomasia kurejesha kiwanja cha Malkazi
Chang’ombe kwa kuzingatia kuwa itatatua mgogoro huo katika njia nyepesi”
alidai Sheikh Ponda.
Alidai Sheikh Ponda.Nyerere sasa tusilete mijadala isiyokuwepo.”
Hata
hivyo, Sheikh Ponda alikubali kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliohusika
kutoa taarifa kwa maimamu wa misikiti mbalimbali kuwaeleza waumini wao
kushiriki kujitolea katika ujenzi wa msikiti wa muda uliojenga katika
eneo la Malkazi Chang’ombe Oktoba 11 na kukamilika Oktoba 14, mwaka
jana.
Alidai
kuwa walijenga msikiti huo baada ya kufanya makubaliano na mmoja wa
wamiliki wa Kampuni ya Agritanza Ltd, Hafidhi, na kukubaliana kuweka
alama ambayo kila Muislamu akiiona ataiheshimu na kutofanya shughuli
zake binafsi katika eneo hilo na kupendekeza kujenga msikiti huo wa
muda.
Kuhusu kukamatwa kwake.
Sheikh
Ponda alidai kuwa yeye alikamatwa Oktoba 16, 2012, nyakati za saa 4
kasoro usiku alipokuwa akijiandaa kuingia katika Msikiti wa Tungi Temeke
, akipanda ngazi alitokea mtu mmoja aliyekuwa kwenye gari nyeusi aina
ya Toyota Harrier akimtaka amfuate.
Post a Comment