Mwenyekiti
wa Simba Al Hajj Ismail Aden RAge akizungumza na wanachama pamoja na
mashabiki wa Simba hii leo mara baada ya kurejea kutoka nchini India
alipokwenda kwa ajili ya matibabu.
Baadhi ya mashabiki wakimsikiliza Rage
Baadhi ya mashabiki wakimsikiliza Rage
Baadhi ya mashabiki wakimsikiliza Rage
Baadhi ya mashabiki wakimsikiliza Rage
Baadhi ya mashabiki wakimsikiliza Rage
Na Dina Ismail
MWENYEKITI
wa klabu ya Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema kuwa chokochoko
zinazoendelea ndani ya klabu hiyo inatokana na tamaa ya dola 300,000 za
mauzo ya aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Emmanuel Okwi aliyeuzwa
katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
Aidha,
Rage amesisitiza kuwa hakuna kitu kinachoitwa mapinduzi ndani ya klabu
hiyo na kwamba anawasubiri kwa hamu leo makao makuu ya klabu hiyo wale
waliotangaza kumpindua.endelea kuifutilia audifacejackson blogspot.
Akizuingumza
na mashabiki na wanachama wa klabu hiyo jioni ya leo makao makuu ya
klabu mitaa ya Msimbazi na Twiga mara baada ya kurejea kutoka nchini
India alipokwenda kwa matibabu, Rage alisema wanaoleta matatizo ndani ya
klabu hiyo ni wale wenye utu wa kujil;imbikizia mali.
Alisema
chini ya uongozi wake Simba imefanya mambo ya uwazi na ukweli ikiwamo
hilo suala la kuuza wachezaji ambapo fedha zimeonekana tofauti na
waliomtangulia kwani walipowuza wachezaji ferdha ziliyeyuka.
“Tumemuuza
Samata (Mbwana) , tumemuuza Ochan (Patrick) fedha zimeoonekana lakini
je wao walipowauza kina Henry Joseph, Haruna Moshi (Boban), Danny
Mrwanda, na wengineo klabu ilipata sh ngapi?
Rage
aliongeza kuwa chini ya uongozi wake wamewezesha kupatikana kwa fedha
kupitia kodi ya pango ya jengo hilo ambapo awali ilikuwa sh 200,000
lakini sasa imepanda hadi milioni 2 na hiyo pia ni sababu inayowapa
tamaa watu hao weasioitakia mema.
Akienda
mbali zaidi Rage alisema kama kundi hilo lililofanya mapinduzi lingekuwa
halali hata watu wqaliowateua kuongoza kwa muda Zacharia Hans Poppe na
Rahma Al Kharoos ‘Malikia wa Nyuki’ wasingewakatalia kukalia hayo
madaraka yao ya muda.
Rage
alisema kwa sasa uongozi umedhamirtia kuiletea mafanikio timu hiyo
kongwe kama huku akisema ni aibu kwa hali iliyonayo pamoja na ukongwe
huo ukilinganishga na Azam hayo jana kwenye makao makuu ya klabu hiyo
mara baada ya kuwasili kutoka nchini India alipokwenda kwa ajili ya
matibabu.
“Angalia
Azam ina miaka 10 tu katika ulimwengu wa soka ina mafanikio makubwa,
lakini Siumba ina miaka 70 hakuna cha maana tyulichofanya lazima tuone
aibu,”aliongeza
Hivi
karibuni zaidi ya mashabiki 700 wa timu hiyo waliitisha mkutano mkuu wa
dharula na kuadhimia kumng’oa Rage na wenzake kwa madai ya kushindwa
kuiongoza klabu hiyo kiasi cha kufanya timu ya Simba kufanya vibaya
kwenye mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom kabla ya kutolewa katika hatua
ya pili ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Read more: http://audifacejackson.blogspot.com
Post a Comment