|
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk. Norman
Sigalla |
|
KAMATI ya Ulinzi na
Usalama Mkoa wa Mbeya limepiga marufuku maandamano yoyote kufanyika Mkoani hapa
yenye lengo la kushinikiza Raisi Kikwete kumfukuza kazi Waziri wa Elimu kutokana
na matokeo mabaya ya kidato cha nne.
Maandamano hayo
yalipangwa kufanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) Machi 25,
Mwaka huu, ambayo yamepangwa kuhusisha Mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini na
kufanyika Jijini Mbeya kwa lengo hilo.
Akitoa taarifa ya
Kamati hiyo kwenye Mkutano wa ushauri wa Mkoa (RCC),Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Dk. Norman Sigalla amesema kamati hiyo ilikaaa Machi 19, mwaka huu na kuamua
kuwa hakuna mantiki ya kufanyika kwa maandamano
hayo.
Amesema sababu
iliyoonekana ni kwamba tayari tume imeshaundwa kuchunguza madai hayo hivyo hamna
sababu ya watu kuandamana kushinikiza waziri kujiuzulu ili hali kamati itakuja
na majibu juu ya kile kilichosababisha matokeo kuwa
mabaya.
Sigalla amesema kamati
ya Ulinzi na Usalama imeona kuwa kuendelea kufanya maandamano soyo ufumbuzi wa
matatizo bali yataathiri shughuli za kujitafutia kipato kwa wananchi wa kawaida
pamoja na usalama wa mali.
Ameongeza kuwa usalama
wa Wananchi wa Mkoa wa Mbeya utaathirika kutokana na wanaotarajiwa kufanya
maandamano hayo wamehamasishwa kutoka mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma ambako
kutajaza idadi kubwa ya watu.
Amesema kamati pia
inaamini kuwa maandamano ya aina hiyo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani
hivyo kamati inapiga marufuku maandamano ya aina yoyote kufanyika Mkoani Mbeya
na kuongeza kuwa yapelekwe maeneo mengine.
Aidha ametoa rai kwa
vikundi vya kisiasa, kijamii na vikundi vya dini kuweka mbele maslahi ya
wananchi kwa kuhimiza kujitafutia vipato kutokana na fursa za maendeleo
zilizopo.
Hata hivyo Mwenyekiti
huyo wa kamati ya Ulinzi na Usalamaya Mkoa ameviagiza vyombo vyote vya Ulinzi na
usalama kuendelea kuhakikisha kwamba Mkoa wa Mbeya unaendelea kuwa tulivu na
amani ambayo itawezesha wananchi kuendelea na shughuli za kujiongezea kipato
bila bugudha yoyote.
Maandamano hayo
yamepangwa kufanyika Machi 25, Mwaka huu kufuatia Mkutano wa Hadhara uliofanyika
hivi karibuni wa Chadema katika Viwanja vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe Ilomba
Jijini Mbeya Februari 28, Mwaka huu, ambapo Mwenyekiti wa Chama hicho taifa
Freeman Mbowe aliagiza kufanyika kwa maandamano hayo kwa namna yoyote
ile.
Pia katika kuhakikisha
dhana hiyo inatimia Mwenyekiti huyo pia alichangisha zaidi ya Shilingi Milioni
Tatu ambazo alidai kuwa zitasaidia wakati wa maandamano katika kununulia maji ya
kunawa baada ya kupigwa na mabomu pia kununulia dawa za huduma ya kwanza kwa
watakaoathirika na maandamano
hayo.
|
on Saturday, March 23, 2013
Post a Comment