***********
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alisema jana kuwa ujenzi huo
unaofanywa na Kampuni ya China Petroleum and Technology Development Co-operation
(CPTDC), ambao awali, ulipaswa kuanza wiki iliyopita, umeanza juzi baada ya
Serikali kufikia mwafaka na wananchi wa Kijiji cha Msimbati
kinapojengwa.
“Mkuu wa Wilaya
ya Mtwara (Wilman Ndile) na vijana wake walilazimika kufika Kijiji cha Msimbati,
ambako wananchi walikuwa na mgogoro na watu wa Marine Park,” alisema
Maswi.
Alisema baada ya
ziara hiyo kushindwa kufanyika Jumapili iliyopita, uongozi wa wilaya ulikutana
na viongozi wa kijiji na kufikia mwafaka uliofanikisha kuanza kwa ujenzi
huo.
Alisema kuanzia
mradi huo kutatoa ajira za kawaida kwa wakazi saba wa maeneo yanayozunguka mradi
huo na kwamba kazi hiyo itaongeza mahitaji ya bidhaa mbalimbali na huduma katika
Kata ya Msimbati
“Mathalan kuku,
matunda na mboga za majani vinahitajika sana. Sasa wananchi ambao awali,
hawakutaka kuelezwa lolote, wameanza kuchangamkia fursa hizo jambo ambalo
litawanufaisha zaidi,” alisema.
Ujenzi huo
ulielezwa kuwa unatekelezwa sambamba na mwekezaji kujenga visima vitatu vya maji
safi na salama kijijini Madimba.
Alisema
mwekezaji pia atasambaza umeme kwa kaya 300 za ndani na jirani ya kijiji hicho
na kwamba vifaa vitakavyotumika katika kazi hiyo vinatarajiwa kuwasili mwishoni
mwa mwezi huu.
Maswi alisema
shule zote kwenye Kata ya Msimbati kikiwamo Kijiji cha Madimba, zitakarabatiwa
na mwekezaji huyo ikiwa ni sehemu ya mpango wa wananchi waishio maeneo ya mradi
kunufaika na uwekezaji.
Hata hivyo,
habari nyingine zinaeleza kuwa ulinzi umeimarishwa katika eneo hilo la mradi ili
kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuwapo.
Mwananchi
Mwananchi
Post a Comment