Waziri Mkuu akihutubia leo asubuhi |
Azindua tume ya watu 15,
aipa wiki sita kukamilisha kazi
*************
WAZIRI MKUU Mizengo
Pinda amezindua Tume maalum aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa
matokeo ya mtihani wa
kidato cha nne yaliyotangazwa Februari 18, mwaka huu na
kuwataka wajumbe wa Tume
hiyo watafute kiini cha mserereko wa kushuka kwa
ufaulu kuanzia mwaka
2010 hadi 2012.
Ametoa kauli hiyo leo
asubuhi (Jumamosi, Machi 2, 2013) wakati akizungumza na wajumbe
wa
Tume hiyo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar
es
Salaam. Mkutano huo
ulihudhuriwa pia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Dk. Shukuru
Kawambwa.
“Nimetafuta takwimu za
tangu mwaka 2005, Serikali ya Awamu ya Nne ilipoingia madarakani
na
kubaini kuwa tangu
wakati huo hadi mwaka 2009 tulikuwa tukifanya vizuri, lakini
kuanzia mwaka 2010 hadi
2012 matokeo yamekuwa yakishuka sana,” aliwaambia
wajumbe wa Tume hiyo na
waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
Alisema hali hiyo
haikuwa kwenye shule za sekondari za umma (kata) peke yake bali
hata
kwa shule za Serikali,
za watu binafsi na kwenye seminari ambazo kwa miaka
Akitoa mfano, Waziri
Mkuu alisema: “Mwaka 2005 kiwango cha ufaulu kilikuwa asilimia
89.3; mwaka 2006
asilimia 89.12; mwaka 2007 asilimia 90.6; mwaka 2008 asilimia
83.6 na mwaka 2009
asimilia 72.5, hapa napo tulikuwa bado tuko vizuri japo si
sana ikilinganishwa na
miaka mine iliyotangulia.”
“Lakini mwaka 2010,
kiwango cha ufaulu kilishuka na kufikia asilimia 50.4, mwaka
2011
kilipanda kidogo na
kufikia asilimia 53.6 na kilishuka zaidi mwaka jana ambapo
kilifikia asilimia 34.5.
Hapa ni lazima mtu utapata maswali ya msingi na kujiuliza
nini kimetokea katika
miaka ya hivi karibuni,” alisema.
Waziri Mkuu alibainisha
kwamba idadi ya watahiniwa iliongezeka kutoka 85,292 mwaka 2005 na kufikia
248,336 katika mwaka 2009 wakati idadi ya walimu nayo pia iliongezeka kutoka
20,414 na
kufikia 37,218 katika
kipindi hichohicho.
Alisema anatambua
changamoto nyingine zinazoikabili sekta ya elimu kama vile uhaba wa vitendea
kazi, upungufu wa maabara na walimu wa sayansi, upungufu wa mabweni pamoja na
nyumba za
walimu.
Kinachoshangaza, Waziri
Mkuu alisema, mbali na kuongezeka kwa walimu kutoka 44,053 mwaka 2010, walimu
55,982 (mwaka 2011) na kufikia walimu 68,784 mwaka 2012 bado kiwango cha ufaulu
nacho
kilikuwa kikishuka
katika kipindi hichohicho.
Akitoa mfano, Waziri
Mkuu alisema: “Kwenye shule za kata, mwaka 2010, walifaulu wanafunzi 114,883;
mwaka 2011 wanafunzi 106,286 na mwaka 2012 wanafunzi 74,817 wakati kwenye shule
za Serikali, katika kipindi hicho hicho ufaulu ulishuka kutoka wanafunzi 19,412,
na kufikia wanafunzi
10,712.”
Waziri Mkuu alisema
katika mchanganuo huo, jambo moja kuu lililo bayana ni kuwepo kwa mzao wa kwanza
wa shule za kata katika mwaka 2010 lakini bado athari za kushuka kwa ufaulu
zikasambaa
kote hadi kwenye shule
za serikali, za binafsi na seminari.
Akianisha kushuka kwa
ufaulu wa daraja la kwanza katika makundi hayo, Waziri Mkuu alisema: “Mwaka
2010, kwenye shule za kata, walifaulu wanafunzi 1,225 wakati mwaka 2011 walikuwa
wanafunzi 564 na mwaka 2012 walikuwa wanafunzi 162”.
“Kwenye shule za
Serikali, mwaka 2010, walifaulu wanafunzi 952, mwaka 2011 wanafunzi 771 na mwaka
2012 wanafunzi 253. Kwenye shule za binafsi, mwaka 2010, walifaulu wanafunzi
2,476 mwaka 2011 Wanafunzi 1,614 na mwaka 2012 wanafunzi 1,032. Kwenye seminari,
mwaka 2010, walifaulu wanafunzi 695, mwaka 2011 wanafunzi 428
na
mwaka 2012 wanafunzi
197.”
Akianisha matokeo ya
waliofeli kwa kupata daraja ‘0’, Waziri Mkuu alisema: “Mwaka
2010,
kwenye shule za kata,
walifeli wanafunzi 151,848 wakati mwaka 2011 walifeli
wanafunzi 143,552 na
mwaka 2012 walifeli wanafunzi 223,774”.
“Kwenye shule za
Serikali, mwaka 2010, walifeli wanafunzi 7,926, mwaka 2011 wanafunzi
9,790
na
mwaka 2012 wanafunzi 16,176. Kwenye shule za binafsi, mwaka 2010, walifeli
wanafunzi
13,346 mwaka 2011
wanafunzi 16,620 na mwaka 2012 wanafunzi 25,055. Kwenye
seminari,
mwaka 2010, walifeli
wanafunzi 638, mwaka 2011 wanafunzi 972 na mwaka 2012 wanafunzi
1,329.”
Alisema kwa mujibu wa
hadidu za rejea, wajumbe wa tume hiyo watatakiwa kuangalia ni sababu zipi
zimechangia kuwepo kwa matokeo hayo mabaya, mserereko wa kushuka umekuwa
ukiongezeka kwa sababu gani,usimamizi katika Halmashauri ukoje, ukaguzi wa elimu
na uhamishiwaji wa sekta
ya
elimu kwenye Wizara ya TAMISEMi umechangiaje kushuka kwa kiwango cha
ufaulu.
Vilevile, watatakiwa
kuangalia mitaala na mihutasari ikoje, kuangalia uwiano uliopo
kwenye mitihani
inayotungwa ikiwa ni pamoja na uhakiki wa mitihani hiyo;
kuangalia
mazingira ya
kufundishia, mfumo wa upimaji, usimamizi na uendeshaji, na
kutokuwepo
kwa chakula shuleni
kunachangiaje kushuka kwa utendaji mbaya wa wanafunzi
katika masomo
yao.
Tume hiyo yenye wajumbe
15, imepewa muda wa wiki sita kuanzia Machi mosi iwe
imekamilisha
kazi hiyo na kuwasilisha
taarifa yao kwa Waziri Mkuu. Itaongozwa na Prof.
Sifuni Mchome wa Tume ya
Vyuo Vikuu, na Makamu wake atakuwa Bi. Bernadetha
Mushashu (Mbunge wa Viti
Maalum – Kagera).
Wajumbe wengine ni Bw.
James Mbatia (mbunge wa Kuteuliwa), Bw. Abdul J. Marombwa
(Mbunge
wa
Kibiti), Prof. Mwajabu Possi (Chuo Kikuu - UDSM), Bibi Honoratha Chitanda
(CWT)
na
Bibi Daina Matemu (TAHOSSA) na Bw. Mahmoud Mringo (TAMONGSCO).
Wengine ni Bw. Rakhesh
Rajani (TWAWEZA), Bw. Peter Maduki (CSSC), Mwl. Nurdin Mohamed
(BAKWATA), Bw. Suleiman
Hemed Khamis (Baraza la Wawakilishi), Bw. Abdalla Hemed
Mohamed (Chuo Kikuu –
SUZA), Bw. Mabrouk Jabu Makame (Baraza la Elimu Z’bar na
Bw. Kizito Lawa (Taasisi
ya Kukuza Mitaala)
(mwisho)
IMETOLEWA
NA:
OFISI YA WAZIRI
MKUU,
S.
L. P 3021,
DAR ES
SALAAM.
JUMAMOSI, MACHI 2,
2013.
Post a Comment