Mwili wa Jambazi sugu Emanuel Blasius Mdendemi ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani akiangalia mwili jambazi lililouwawa na kikosi cha polisi Mbeya
Baadhi ya polisi na waandishi wa habari wakiwa nje yajengo la kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa Mbeya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika Mkutano alioufanya na waandishi wa Habari Ofisini kwake ambapo alisema tukio hilo lilitokea jana majira ya Saa 10(kumi) Alfajiri
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akionyesha baadhi ya siraha alizokutwanazo jamabazi huyo aliyeuwawa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akionyesaha hirizi iliyofungwa katika bunduki aliyokuwa anatumia jambazi huyo kama kinga katika matukio yake
Hii ndiyo hirizi iliyofungwa katika bunduki aliyokuwa anatumia jamabazi huyo jamani waganga wakienyeji acheni hizo kuwadanganya watu matokeo yake ni kuongeza uhalifu nchini hakika nao tutawashughulikia kwani wamekuwa chanzo cha uhalifu nchini hayo yamesemwa na kamanda Diwani
Kamanda Diwani akiongea na waandishi wa habari
MTU mmoja ambaye anasadikiwa kuwa ni jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari wa Jeshi la Polisi akiwa kwenye harakati za kuteka magari katika Eneo la Mlima Nyoka Jijini Mbeya baada ya kutokea kwa majibizano ya kurushiana risasi.
Jambazi huyo ni
miongoni mwa watu waliokuwa wakitafutwa na Jeshi la Polisi Mkoani hapa
akituhumiwa kuhusika na mauaji ya Askari Polisi mwenye namba G 68 PC Jafari
yaliyotokea Februari 6, Mwaka huu katika eneo la Matundasi Wilayani
Chunya.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika
Mkutano alioufanya na waandishi wa Habari Ofisini kwake ambapo alisema tukio
hilo lilitokea jana majira ya Saa 10(kumi) Alfajiri
Kamanda Diwani
alisema kabla ya tukio majambazi wapatao wanne tayari walikuwa wameweka mawe
barabarani kwa nia ya kuteka magari ili wafanye uporaji katika eneo hilo la
Mlima Nyoka ambalo limekuwa na matukio kadhaa ya watu kuporwa mali
zao.
Alisema Jeshi la
polisi baada ya kupata habari za kutegwa mawe, askari walifika kwa wakati kwa
kuwa polisi walikuwa jirani na eneo hilo na kuweka mtego kwa kuwa majambazi
hawakuwa wameonekana kwa wakati ule.
Aliongeza kuwa
baada ya muda majambazi walipoona taa za gari walijitokeza tayari kushambulia
lakini kabla ya hapo polisi walitoa amri ya kujisalimisha kinyume chake wakaanza
kupiga risasi ovyo ndipo mashambulizi ya polisi yakafanywa.
Diwani alisema
katika mapambano hayo alijeruhiwa jambazi mmoja kwa risasi kiunoni na ubavuni
kulia na wengine watatu walifanikiwa kutoroka ambapo Marehemu alipowahishwa
hospitali kwa matibabu daktari alibaini kuwa amekwisha fariki.
Alisema jambazi
huyo alikutwa na silaha moja SMG yenye namba AB huku namba nyingine zikiwa
zimefutwa na magazine yake ikiwa na risasi ishirini na mbili (22) pamoja na
mapanga mawili([2).
Aliongeza kuwa
baada ya Marehemu kufanyiwa upekuzi maungoni mwake jambazi huyo alikutwa na
kitambulisho cha mkazi chenye namba B.0010453 chenye jina la Emanuel Blasius
Mdendemi aliyezaliwa mwaka 1984 eneo la Matamba wilayani Makete Mkoa wa Iringa
makazi yake ni Uwemba Mkoani Njombe.
“Jambazi huyu
amebainika kuwa ni miongoni mwa majambazi waliokuwa kwenye mtandao wa majambazi
uliokamatwa hivi karibuni kuhusiana na matukio waliyofanya Mikoa mbalimbali
ikiwemo Mbeya,Njombe na Iringa.aidha amebainika kushiriki katika tukio la mauaji
ya askari polisi PC Jafari wa kituo cha Mkwajuni – Chunya tarehe 06.02.2013.”
Alisema Kamanda Diwani.
Aliongeza kuwa
ufuatiliaji wa majambazi waliotoroka unaendelea kufanywa ambapo pia anatoa
wito kwa yeyote mwenye taarifa za wahalifu hao azitoe bila kuchelewa kwa jeshi
la polisi ili zifanyiwe kazi.
Pia
amewatahadhalisha majambazi na wahalifu wa makosa yeyote kuachana na uhalifu
kwa kuwa ni biashara isiyo na faida badala yake wafanye shughuli halali kupata
maendeleo ambazo fursa zake ni nyingi.
Picha na Mbeya
yetu
Post a Comment