KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MOROGORO FAUSTINE SHILOGILE.
Na Juma
Mtanda.
JESHI la polisi mkoa wa
Morogoro lipo katika wakati mgumu wa kumsaka askari wa hifadhi ya taifa ya
wanyamapori ya Mikumi kwa tuhuma za kufyatua risasi iliyomlenga mfugaji, Muri
Sityo (23) kisogoni na kufariki dunia papo hapo kisha mwili wake kutupwa sehemu
ambayo haijajulikana mkoani Morogoro.
Tukio hilo linadaiwa
kutokea marchi 1 mwaka huu majira ya saa 6 mchana wakati mfugaji huyo akinywesha
maji mifugo na wenzake katika bwawa lililopo ndani ya hifadhi hiyo jirani na
mpaka wa kijiji cha Mkata-Luhoza wilaya ya Kilosa mkoani hapa.
Akizungumza na gazeti
hili katikati ya wiki mjini hapa katika mahojiano maalum, Kamanda wa polisi mkoa
wa Morogoro, Faustine Shilogile alisema kuwa ni kweli jeshi la polisi linamska
askari wa hifadhi ya taifa ya wanyamapori ya Mikumi kwa tuhuma za kufyatua
risasi na kusababisha kifo cha mfugaji, Muri Sityo kufariki dunia papo hapo
marchi 1 mwaka huu mkoani hapa.
Shilogile alisema kuwa
jeshi la polisi hivi sasa lipo katika uchunguzi wa kina wa tukio hilo kwa
kumsaka askari na pamoja na kuchukua sampori ya tope lililochanganyikana na damu
kwa ajili ya kupimwa kwa mkemia mkuu wa serikali ili kuweza kubaini ukweli wa
tukio hilo ambalo mpaka sasa limekubikwa na utata kutokana na mazingira ya tukio
lenyewe ikiwemo mwili wa marehemu kutokutwa eneo la tukio .
Nilituma askari kwenda
eneo la tukio lakini walipofika hawakuweza kuona mwili wa marehemu na badala
yake waliona damu iliyotapakaa katika tope hivyo walichukua tope lenye damu kwa
ajili ya uchunguzi zaidi pamoja na kumsaka mtuhumiwa” alisema
Shilogile.
Aliongeza kwa kusema
kuwa jeshi la tayari limeanza uchunguzi wa awali ikiwemo kuwahoji askari
waliokuwa katika Mbogayaga Ranger Post iliyopo jirani na mpaka wa kijiji
Mkata-Luhoza na hifadhi hiyo.
Akizungumzia juu ya
kutokamatwa kwa mtuhumiwa huyo mpaka sasa, Shilogile alisema kuwa juhudi
zinaendelea kufanywa zikiwemo za kufanya mazungumzo na mkuu wa hifadhi ya taifa
ya Mikumi na kati ya makubaliano yaliyofikiwa ni lazima mkuu huyo anapaswa
kumfikisha mtuhumiwa katika mikono ya jeshi la polisi Morogoro. Alisema
Shilogile.
Shilogile aliendelea
kueleza kuwa taarifa alizonazo juu ya mtuhumiwa huyo ni kuwa yupo likizo jambo
ambalo linawapa kazi katika harakati za kumkamata mtuhumiwa.
Shilogile alimetoa wito
kwa taasisi za zinazohusika na ulinzi ikiwemo na jeshi la polisi kiujumla
kuzingatia zaidi sheria pindi wanamkamata mtuhumiwa kuhakikisha anafikishwa
salama katika vyombo vya dola ili sheria ifuate mkondo wake huku akiwataka
wananchi nao kuzingatia sheria za nchi bila shuruti ili mkoa wa Morogoro na
Tanzania kiujumla uendelea kuwa na amani.
Katika tukio hilo ambalo
lilitokea majira ya saa 6 mchana mwaka huu ndani ya hifadhi ya taifa ya
wanyamapori Mikumi askari wenye cheo cha sajeti (Pius Minja) anadaiwa kufyatulia
risasi na kumpiga mfugaji, Muri Sityo (23) kisogoni na kufariki dunia papo hapo
wakati yeye (marehemu) akimwesha mifugo maji mifugo bwawa lililopo ndani ya
hifadhi hiyo katika mpaka na kijiji cha Mkata-Luhoza kata ya Tindiga Kilosa
Morogoro.
Post a Comment