Jumuiya ya waTanzania DMV imeweza kufanikisha
darasa la kiswahili kwa watoto wao, jumla ya watoto (27) waliweza kuhudhuria
katika darasa lililo funguliwa rasmi siku ya Jumamosi, tarehe 23 March 2013
College Park Maryland Nchini Marekani.
Baadhi ya walimu
waliojitolea kuwasomesha watoto akiwemo Mratibu wa darasa hilo na pia katibu wa
Jumuiya ya Watanzania DMV Bwana Amos Cherehani (Wakwanza kulia) akitoa maelezo
juu ya ufunguzi wa darasa la Kiswahili lililofunguliwa rasmi kwaajili ya watoto,
Siku ya Jumamosi, tarehe 23 March 2013 Callege Park Maryland Nchini
Marekani.
Watoto hao ambao ni wanafunzi wa darasa hilo waliweza kujiandikisha na pia kupangwa kwa makundi kutokana na uelewa wao wa kujua lugha ya Kiswahili na baada ya hapo watoto walijiandikisha na kuazishwa somu la kujua herufi za AEIOU.
Walimu walijitahidi sana kwa watoto waliojiandikisha na baadae kufundishwa kujua kuongea Kiswahili, chini ya Mratibu Mkuu wa darasa hilo bwana Amos Cherehani na kumkaribisha Mgeni rasmi ambae alikua Rais wa Jumuiya ya waTanzania waishio DMV Bwana Iddi Sandaly.

Rais wa Jumuiya ya
waTanzania DMV Bwana Iddi Sandaly akiwakabidhi zawadi wanafunzi waliojiandikisha
katika darasa hilo.
''Nimefurahishwa sana na pia nawashukuru sana wazee pamoja na walimu ambao wameshiriki kwa kujitolea pamoja na wazee kuwaleta watoto wao kwa lengo la kujifunza lugha yetu ya Kiswahili tuko pamoja na tutashirikiana kuendeleza utaratibu huu kwa watoto wetu'', alisema Bwana Iddi Sandaly,
Mpangilio mzima ulioazishwa wakukuza na
kuitunza lugha ya kiswahili kwa watoto wa waTanzania wanaoishi DMV ni kama
ajira kwa watoto wetu alisema Mratibu wa darasa hilo bwana Amos Cherehani ambae
pia ni Katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV
Aidha Mratibu Mkuu wa darasa la kiswahili bwana
Amos Cherehani aliwaomba waTanzania wanaoishi hapa DMV ambao wamebarikiwa kua na
watoto wenye umri wa kwenda shule waje kujiunga na kuwaleta watoto wao kujifunza
lugha ya Kiswahili bila ya malipo.
Baadhi ya watoto wanafunzi waliohudhuria
kujiandikisha katika darasa la kiswahili na kuanza kujifunza kiswahili pamoja na
kuhamasiswa wazee wajitahidi kuwafundisha kujua vitu tafauti kwa majina ya
kiswahili.
Baada ya darasa walimu waliweza kuakabishi
zawadi mbali mbali za kuweza kuwasaidi kujifunza kusoma na kuandika kiswahili
zikiwemo madaftari pamoja na kalamu kwa kila mwanafunzi aliejiandikisha katika
darasa hilo.
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV Amos
Cherehani pamoja na uongozi mzima akihamasisha watoto wanafunzi pamoja na wazee
kuhusu umuhimu wa kuongea lugha ya Kiswahili Ughaibuni ni kama ajira alisema
Mwenyekiti.
Post a Comment