Naungana na Watanzania ambao hatukupata nafasi ya kwenda uwanja wa Taifa kushuhudia timu ya taifa ikitupa raha wengine matokeo tumeyapata kupitia Facebook , tuseme ukweli hii ni aibu tena aibu kubwa kwa tukio hili muhimu ambalo mwisho wa siku linatuunganisha watanzania, kisha TFF na wizara yenye dhamana na michezo mmeshindwa kutuonyesha pambano hili live,
Kama hata mmeshindwa kulipia kurusha matangazo ya mpira kupitia vituo binafsi why Television ya taifa ambalo ina wajibu wa kuwatumikia watanzania, najua wengine watasema kwasababu maalumu labda luninga ya taifa leo ilikuwa na jukumu la kitaifa je hii mechi haikuwa ya kitaifa au kimataifa kama vyote vilikuwa na umuhimu basi sasa kuna umuhimu tukaiona station ya michezo na burudani ikifungulia ikawa stesheni maalumu kwaajili ya michezo na burudani hapa tuweze kuona mechi za kimataifa nchi yetu inavyocheza na mechi za ligi kuu.Kwa leo sina mengi najaribu kuwasamehe kwakuwa timu imeshinda ila next time tunaomba muige mfano hata wa timu Ya Azam ilipokuwa Sudan hivi majuzi tuliweza kuona mechi yao LIVE, faida zipo nyingi sana kuonyesha mechi live Mojawapo ni kuweza kutangaza nchi Yetu kwenye nyanja tofauti kimataifa,
Kuwatangaza wachezaji kimataifa ili angalau kuelekea brazil tuwe na kina samatta hata watano hivi na ni muhimu kama ni timu ya taifa si watu elfu 60 tu wanaotosha kujaza uwanja wa taifa ndio waweze kutazama mpira hata mtu wa bukoba ndanii huko anataka kuona timu yake pia nna hata mtanzania aliyeko kenya anatamani kuiona timu yake maana siku hizi vin'gamuzi kila kona naamini hata kurusha mpira online yawezekana pia ili hata watanzania walio hata bara la ulaya waone timu yetu ikifanya mambo dimbani.Hili ni funzo nadhani kama kuna muhusika wa TFF ameona hii kuna haja ya kuifanyia kazi.
Capt Mkami
lmkami@dudumizi.com
Post a Comment