Mkurugenzi
wa Masoko wa Serengeti Brewries Limited ,Bw.Ephrahim Mafuru akizungumza
jambo mbele ya Waandishi wa habari waliohudhuria katika uzinduzi wa
kampeni mpya ya bia ya Serengeti Premium Lager inayoitwa "TUPO
PAMOJA-KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO,ambayo inatarajiwa kufanyika nchi
nzima katika maeneo mbalimbali na Kampeni hiyo imeanzia Jijini Dar Es
Salaam
Meneja wa Kinywaji cha Serengeti Premium Lager,Bw.Allan Chonjo akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari namna kampeni hiyo "TUPO PAMOJA-KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO",itakavyofanyika katika mikoa yote ya Tanzania
Baadhi wa wageni waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni ya TUPO PAMOJA - KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO iliyozinduliwa leo na kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited wakiangalia moja ya Tangazo Jipya la Kampeni hiyo kwenye screen Kubwa uzinduzi huo umefanyika katika hotel ya JB Belmonte
Baadhi wa wageni waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni ya TUPO PAMOJA - KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO iliyozinduliwa leo na kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited wakiangalia moja ya Tangazo Jipya la Kampeni hiyo kwenye screen Kubwa uzinduzi huo umefanyika katika hotel ya JB Belmonte
Meneja wa Kinywaji cha Serengeti
Bw Allan Chonjo Kwa pamoja na Meneja Masoko wa SBL Bw Ephraimu Mafuru
wakishirikiana kwaajili ya kuweza kuonyesha tangazo la kampeni ya TUPO
PAMOJA - KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO kampeni iliyozinduliwa leo katika
Hotel ya JB Belmonte ya jijini Dar Es Salaam
.........
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) leo imezindua
kampeni mpya za matangazo kuitangaza bia yake maarufu ya Serengeti
inayopendwa na idadi kubwa ya watu. Kampeni hizo maalumu ambazo
zitajulikana kama Tupo Pamoja Katika Shangwe za Mafanikio.
Akizungumza na waandishi wa habari na wageni waalikwa katika
hafla ya uzinduzi wa kampeni hizo jijini Dar es Salaam ndani ya JB
Belmont Hotel, Mkurugenzi wa Masoko SBL, Ephraim Mafuru amesema kampeni
hizo ni maalumu kwa ajili ya kuwashukuru Watanzania ambao wamekuwa
pamoja kiushirikiano katika mafanikio ya kinywaji hicho.
Alisema Watanzania wanahitaji kuthaminiwa hivyo wameona kwa
kuthamini mchango wao kuna kila sababu za kusherehekea katika mafanikio.
"Kampuni ya Bia ya Serengeti inatambua mchango wa kila Mtanzania katika
mafanikio yake...ndiyo maana imezindua kampeni hii ya tupo pamoja
katika shangwe za mafanikio," alisema Mafuru.
Naye Meneja wa Bia ya Serengeti, Allan Chonjo akizungumza
katika hafla hiyo alisema kampeni hizo zinazoanzia Mkoa wa Dar es Salaam
kwa maonesho mbalimbali na burudani zitakuwa zikiendeshwa baa
mbalimbali huku zikiambatana na wateja wa kinywaji hicho kujishindia
zawadi anuai.
Alisema kampeni hizo zitakazoambatana na matangazo kwenye
vyombo vya habari, barabarani pia zitasambazwa katika mikoa anuai ya
Tanzania, huku wapenzi wa SBL kujishindia pia zawadi mbalimbali.
credits: Lukaza Blog
Post a Comment