Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KINANA NA UJUMBE WA CCM WATEMBELEA KIWANDA CHA VIATU CHA TIANJIAN, CHINA


Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifunguliwa mlango na Ofisa wa Kichina, ili kuingia kwenye gari tayari kwa safari ya kuondoka jimbo la Dongguan kwenda uwanja wa wa Kimataifa wa Baiyun, Guangzhou kwa ajili ya kwenda jimbo la Chengdu, Machi 13,2013.
Sarah akiondoka baada ya kuvishwa kitambaa hicho.
Katibu Mkuu wa CCM na ujumabe wake wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha viatu cha Huanjian, Dongguan, China baada ya kutembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) na ujumbe wake, wakionyweshwa maumbo ya namna kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akitazama kiatu, wakati yeye na msafara wake walipotembelea kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China. Wengine kutoka kwa Kinana ni, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Yusuf Mohamed Yusuf.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, wakipata maelezo kwa video, kuhusu kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Titus Kamani (kulia) na Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi, Khamis Suleiman Dadi wakitazama viatu kwenye kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, wakati viongozi hao walipofuatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Vuai Ali Vuai na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro wakiwatazama wafanyakazi wa kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, wakiwajibika na kazi, walipotembelea kiwanda hicho, Machi 13,2013, wakiambatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China
Wafanyakazi wa Kiwanda cha viatu cha Huanjian, Dongguan, wakiwa kazini.
Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, China, akimvisha skafu Ofisa wa Mambo ya Nje wa Jimbo la Dongguan, Sarah Xie, wakati ofisa huyo akiagana na msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Wapili kulia), kwenye hoteli ya Exhibitin Hotel, baada ya Kinana kumaliza ziara yake katika jimbo hilo, Machi 13, 2013 na kwenda jimbo la Chegdu. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhuisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya, Maganga Sengelema na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela na kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi, Khamis Suleiman Dadi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakiondoka kwenye kiwanda cha Huanjian, baada ya ziara yake kwenye kiwanda hicho.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top