KATIBU
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kinyago
cha 'Ujamaa', Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC),
Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada ya mazungumzo yao,
yaliyofanyika leo katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China. Kinana
yupo nchini China na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM kwa ajili ya ziara
ya mafunzo.
Baadhi
ya viongozi wa CCM waliopo katika ujumbe wa Katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Kinana wakiwa ukumbini wakati wa mazungumzo ya Kinana
alipokuwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China
(CPC), Kamati Kuu jimbo la Sichuan, Zhang Ning, baada , Machi 14, 2013,
katika hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China.
KATIBU
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akipewa zawadi ya picha na
Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati Kuu jimbo
la Sichuan, Zhang Ning, baada ya mazungumzo yao, Machi 15, 2013, katika
hoteli ya Jinjiang, mjini Chendu, China.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na baadhi wa wajumbe walioko katika
msafara wake, wakitazama baadhi ya bidhaa zinazouzwa, kwenye eneo la mji
wa Kihistoria ya zaidi ya miaka 100 wa Jin Sha, mjini Chengdu.
Katibu
wa Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi (kulia) akicheza
muziki na mmoja wa wasanii wa kundi linalotumbuiza kwa kupewa fedha
yoyote na anayevutiwa, kwenye eneo la Mji wa Kihitoria ya zaidi ya miaka
100 wa Jin Sha, jijini Chengdu, China.
Hu
Qingzhong akichora katuni kwa ajili ya kuingizw kwenye simu ya mkononi,
katika Kituo Cha Vijana wajasriamali wasomi cha Chengdu.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (aliyefunfa mikono kifuani), na baadhi
ya wajumbe katika msafara wake, wakimtazama kwa makini kijana, Hu
Qingzhong, aliyekuwa akichora katuni kwenye kompyuta kwa ajili ya
kuwekwa kwenye simu za mkononi. Kinana na ujumbe wake walipotembelea
kituo cha Wajasriamali wasomi cha Chengdu-High-Tech zone, jijini
Chengdu, China, Machi 15, 2013. Kinana yupo nchini China na ujumbe huo
kwa ajili ya ziara ya mafunzo. Picha na Bashir Nkoromo.
Post a Comment