Mtunzi
mashuhuri wa vitabu kutoka kampuni ya Mkuki na Nyota, Mzee Walter Bgoya, akikata
utepe pamoja na mtunzi wa kitabu cha 'Kifo ni Haki Yangu', Eric James Shigongo
(kulia) wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika duka la vitabu la
Tanzania Publishing House lililopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam
leo.
Mtunzi wa kitabu cha 'Kifo ni Haki Yangu', Eric James Shigongo,
akiongea na wadau (hawapo pichani) waliofika katika uzinduzi wa kitabu chake
katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House lililopo mtaa wa Samora
jijini Dar.
Mtunzi Eric Shigongo akimpatia kitabu mtunzi mwenziye, mzee Walter
Bgoya.
Mzee Walter Bgoya akiongea na wanahabari wakati wa uzinduzi wa kitabu
cha Eric Shigongo cha 'Kifo ni Haki Yangu'.
Afisa wa polisi Patrick Massawe ambaye pia ni mtunzi mashuhuri wa
hadithi za magazeti nchini, akisainiwa kitabu na Shigongo wakati wa
uzinduzi.
Eric Shigongo (kushoto), akibadilishana mawazo na msomaji wa hadithi
zake, Ahmed El Maamry, wakati akimsainia kitabu.
Eric Shigongo akimsainia kitabu mwanaye, Samwel Shigongo.
Eric Shigongo akisaini kitabu
kwa ajili ya mwandishi wa Nipashe, Somoe Ng'itu.
Shigongo akiwasainia vitabu baadhi ya wasomaji waliohudhuria uzinduzi
huo.
Waratibu wa uzinduzi wa kitabu cha 'Kifo ni Haki Yangu', Abdallah
Mrisho (kulia) na Angela Msangi wakisubiri uzinduzi.
Afisa wa polisi Patrick Massawe na msomaji mwingine wakipitia baadhi
ya kurasa za kitabu cha Eric Shigongo aliyesimama kulia.
Baadhi ya wasomaji waliohudhuria uzinduzi huo.
Shigongo akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa duka la
TPH.
MTUNZI mahiri wa vitabu nchini, Eric James Shigongo,
leo amezindua rasmi kitabu chake cha 'KIFO NI HAKI YANGU' katika duka la vitabu
la Tanzania Publishing House (TPH) lililopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo, wasomaji 50 wa mwanzo walipata fursa ya kupata zawadi ya
kitabu hicho bure kilichosainiwa na mtunzi. Kujipatia nakala ya kitabu hicho na
vinginevyo, wasiliana au fika katika vituo tajwa hapo chini:
PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL
Post a Comment