Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KONGAMANO LA KUJADILI RASIMU YA SERA YA MANUNUZI YA UMMA LAFANYIKA DAR


Kamishna wa Idara ya Sera ya manunuzi ya Umma, kutoka Wizara ya Fedha Dk. Frederick Mwakibinga (kulia) akizungumza jambo na mjumbe wa kamati ya sera ya manunuzi, Clemence Tesha, wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyoka jana jijini Dar es Salaam leo. Kongamano hilo la siku moja lilihudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
Emmanuel Maliganya ambaye ni Afisa Ugavi kutoka Benki Kuu ya Tanzania akichangia mada kuhusu utendaji kazi wa maafisa ugavi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyoka jana jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
Juma Fimbo kutoka Umoja wa wataalamu wa Manunuzi na Ugavi Tanzania akielezea jinsi maafisa ugavi wanavyotakiwa kufanya kazi zao kwa kutumia taaluma ya uchumi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma.
Mkurugenzi wa Ugavi kutoka Akaunti ya Changamoto za Milinia (Millenium Challange Account) Marieth Ngaida akichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Kamishna wa Idara ya Sera ya manunuzi ya umma kutoka Wizara ya Fedha Dk. Frederick Mwakibinga (kushoto) akisalimiana na Prof. Gaspar Munishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja lilihudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.
Prof. Gaspar Munishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala akielezea kuhusu rasimu ya Sera ya manunuzi wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya wajumbe kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi wakimsikiliza Prof. Gaspar Munishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala (hayupo pichani) wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Khamisi Tikka kutoka Mamlaka ya Rufaa za zabuni akichangia mada wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika jana katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam.Picha zote na Anna Nkinda-MAELEZO
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top