Naibu
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala, akimkabidhi kombe
la Ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup naodha wa timu ya Jambo Leo, Said
Mwishehe, baada ya timu hiyo kuifunga Changamoto bao 1-0 katika mchezo wa
fainali uliochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala, akimkabidhi kombe
la Ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup naodha wa timu ya Business Times
'Business Queens', Lulu Habibu, baada ya timu hiyo kuifunga TBC jumla ya mabao
39-18 katika mchezo wa fainali uliochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa TCC
Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji
wa Jambo Leo, Julius Kihampa, akichuana kuwania mpira na beki wa Changamoto,
Emmanuel Balele, wakati wa mchezo huo wa Fainali uliochezwa leo asubuhi kwenye
Uwanja wa Tcc Chang'ombe. Katika mchezo huo Jambo Leo imeibuka na ushindi wa bao
1-0 na kutangazwa kutwaa kombe hilo la NSSF CUP 2013 na kuwa bingwa mpya wa
michuano hiyo iliyomalizika leo.
Beki
wa Jambo Leo, Mohamed Akida, akimdhibiti kiungo mshambuliaji wa Changamoto,
Hamad Ganichiaga, wakati wa mchezo huo.
Beki
wa Jambo Leo, Mohamed Akida, akiruka kuokoa moja ya hatari langoni
kwake.
Kiungo
Mshambuliaji wa Changamoto, Hamad Ganichiaga (kulia) akijaribu kumtoka beki wa
Jambo Leo, Mansour Mohamed, wakati wa mchezo huo.
Beki
wa Jambo Leo, Mansour Mohamed (kushoto) akimdhibiti Kiungo Mshambuliaji wa
Changamoto, Hamad Ganichiaga, wakati wa mchezo huo.
Beki
wa Changamoto, Emmanuel Ganichiaga, akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa
Jambo Leo, Zahor Milanzi, wakati wa mchezo huo.
Kipa
wa Jambo Leo, akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
Julius
Kihampa (chini) akicheza takorling....
Kina
Dada wa Jambo Leo, wakiwahamasisha kaka zao.
Benchi
la Ufundi la Changamoto na wachezaji wa akiba.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo,
Amosi Makala, akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi
wengine.
Benchi
la Jambo Leo. NA SUFIANI MAFOTO
Post a Comment