Kufikia
sasa asilimia 42 ya kura za urais nchini Kenya zimehesabiwa na kuwasilishwa
rasmi kwa tume ya uchaguzi IEBC kupitia mitambo ya electroniki.
Hata
hivyo kumekuwepo malalamishi kuhusu kucheleweshwa kwa shughuli ya kujumlisha
kura kutokana na hitilafu ya mitambo. Uhuru Kenyatta, anayekabiliwa na kesi
katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC, angali anashikilia uongozi huku kura
za urais zikiwa bado zinahesabiwa.
Huu
ni uchaguzi mkuu wa kwanza kufanyika tangu ghasia za baada ya mwaka 2007/2008
kufuatia matokeo yaliyozua utata.
Kenyatta
aliendelea kuwa mbele kwa hesabu ya matokeo ya mwanzo dhidi ya mpinzani wake
waziri mkuu Raila Odinga katika siku ya pili ya shughuli ya kuhesabu kura zaidi
ya masaa 36 baada ya shughili ya upigaji kura kukamilika. Hadi sasa Uhuru ana
kura milioni mbili nukta nane wakati Raila Odinga akiwa na kura milioni mbilii
nukta mbili
Raila
Odinga alidai kuibiwa ushindi wake mwaka 2007 wakati matokeo yalizua ghasia na
kusababisha vifo vya watu zaidi ya laki moja huku maelfu wakiachwa bila makao. Wakati
mamilioni ya wakenya walijitokeza kupiga kura kwa amani siku ya
Jumatatu,watavyopokea matokeo ya mwisho ya kura ndio itakuwa ishara ya uthabiti
wa nchi hiyo.
Ni
asilimia arobaini na moja ya kura zilizohesabiwa huku kukiwa na vituo zaidi ya
elfu thelathini ambako kura zilipigiwa. Ni zaidi ya kura milioni tano
zilizohesabiwa kutoka kwa wapiga kura milioni 14.3 waliokuwa wamesajiliwa.
Post a Comment