Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na
wananchi Mji mpya wa Mabwe Pande (hawapo pichani) wakati alipofika katika mji
huo jana Machi 14, 2013 akiwa katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi
ya Maji inayosimamiwa na Dawasa na kutembelea katika Mtambo wa Ruvu Chini
kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo huo wa Ruvu chini. Kulia ni
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky
Saidik.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kushoto)
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa miradi ya Maji, William Kazenga,
kuhusu upanuzi wa mtambo wa Ruvu chini wa kusambaza maji, wakati Makamu
alipofika eneo hilo jana Machi 14, 2013 kwa ajili ya kukagua kazi zinazoendelea
za upanuzi wa Mtambo huo wa Ruvu chini.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi wa miradi ya Maji, William Kazenga, kuhusu upanuzi wa
mtambo wa Ruvu chini wa kusambaza maji, wakati Makamu alipofika eneo hilo jana
Machi 14, 2013 kwa ajili ya kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo huo
wa Ruvu chini. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi (wa pili
kushoto) ni Waziri wa Maji na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea kukagua
kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu chini jana Machi 14,
2013 wakati Makamu alipofika eneo hilo jana.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Said Mecky Sadik, Waziri wa Maji, Jumanne Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa
Pwani, Mwantum Mahiza na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, wakiwa katika
picha ya pamoja na wafanyakazi na viongozi wa Dawasa baada ya Makamu kutembelea
na kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo wa Ruvu chini, jana Machi 14,
2013. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Post a Comment