Kwa
ufupi
SERIKALI ya Malawi
imesema ina wasiwasi kuhusu hatma ya mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa na kwamba
hali hiyo inatokana na Tanzania kuvunja sehemu ya makubaliano ya
usuluhishi.
****

Kauli hiyo inakuja
wakati jopo lo viongozi wastaafu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika(Sadc), likijiandaa kuwasilisha ripoti yake baadaye mwezi
huu.
Jopo hilo linaloongozwa
na Rais Mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chissano, litakabidhi ripoti hiyo kwa
viongozi wakuu wa nchi zote mbili.
Waziri wa Mambo ya Nchi
za Nje wa Malawi, Ephraim Chiume, ameituhumu Tanzania kwamba imeanza kuzungumzia
utatuzi wa mgogoro huo wakati ikijua kuwa mzozo huo uko katika hatua ya
upatanishi maalumu.
Waziri Chiume aliikosoa
kauli iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kuwa ufumbuzi wa mgogoro wa mpaka baina
ya mataifa hayo mawili, unakaribia kupatikana.
Alisema kitendo cha
Membe kuzungumzia maendeleo ya mgogoro huo kinapingana na makubaliano ya pamoja
yaliyowasilishwa kwa Chissano na kwamba hatua hiyo inavunja
moyo.
Waziri Chiume aliliambia
gazeti la Nyasa Times kuwa pande zote mbili zilipokutana Nombemba 17 mwaka jana
jijini Dar es Salaam, zilikubaliana kuzungumzia mgogoro huo ili kuepuka
kuingilia juhudi za upatanishi. Alisema hata hivyo, hivi karibuni ya Serikali ya
Tanzania imekiuka sehemu ya makubaliano hayo.
“Tanzania wamevunja
makubaliano, na sisi tunasisitiza kuwa Ziwa Nyasa ni la Malawi,” alisema
waziri.
Baadhi ya wachambuzi wa
mambo, wamesema kauli huyo inaashiria kuwa huenda pande hizo mbili zikashindwa
kukubaliana na mapandekezo yatakayowasilishwa na mpatanishi wa mzozo
huo.
Mpatanishi huyo mwezi
huu anatazamiwa kukutana na Rais Jakaya Kikwete na yule wa Malawi, Joyce
Banda.
Hata hivyo,
alivyotafutwa ili kuzungumzia malalamiko hayo, waziri Membe kupatikana, lakini
Naibu wake Mahadhi Maalimu, alisema: “Ninachosema mimi kwanza hizo taarifa
sijazipata na kama zipo basi Serikali itawasiliana kupitia mikondo sahihi.
Serikali haiwezi kujibizana kupitia magazeti”
Hivi karibuni Serikali
ya Tanzania na Malawi zilipeleka barua ya pamoja kwenye Jukwaa la Marais wa
Wastaafu wa Nchi za Kusini mwa Afrika linaloongozwa Chissano, zikiomba
zipatanishwe katika mzozo huo.
Hatua hiyo ilikuja
baada ya majadiliano ya pande zote mbili kushindwa kuzaa
matunda.
Kama sehemu ya kuepusha
mgongano wa kimaslahi, jopo hilo la wasuluhishi halikuwahusisha viongozi
wastaafu wa Tanzania Alhaji Ali Hassani Mwinyi na Benjamin
Mkapa.
Hali kadhalika Bakiri
Muluzi wa Malawi.
Hata hivyo, duru za
kidiplomasia mjini Lilongwe zinasema Serikali ya Malawi imejiandaa kwenda
katika Mahakama ya Haki ya Kimataifa(ICJ) kama upatanishi huo utashindwa kuzaa
matunda.
Gazeti la Daily Times
limewanukuu maofisa wa Serikali wakisema kuwa karata ya mwisho kwa Malawi
itakuwa ni kwenda katika mahakama
hiyo.

Post a Comment