Kwa
ufupi
POLISI katika Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, imetoa masharti ya kuruhusu maandamano ya amani ya
kupinga kauli ya kashfa iliyotolewa na raia mmoja wa Uingereza, dhidi ya
viongozi wakuu wa nchi.
*********
POLISI katika Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam, imetoa masharti ya kuruhusu maandamano ya amani ya
kupinga kauli ya kashfa iliyotolewa na raia mmoja wa Uingereza, dhidi ya
viongozi wakuu wa nchi.
Maandamano hayo
yaliyoandaliwa na Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya Human Settlements of Tanzania
(Huseta), yamepangwa kufanyika Jumatano na yataanzia Viwanja vya Mnazi Mmoja na
kuishia nje ya Ubalozi wa Uingereza hapa nchini.
Hata hivyo,
Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema
hajapata barua ya kuomba kufanyika kwa maandamano hayo. “Lakini nitaangalia
maudhui, kama yanafanana na maandamano husika,”
alisema.
Alisema akifika
ofisini leo na kuiona barua ya kuomba kufanyika, maandamano hayo atakuwa katika
nafasi nzuri ya kuzungumzia maandamano hayo.
“Nikipata barua
ya maandamano hayo na kuona maudhui yake, nitakuwa katika nafasi ya ama
kuyaruhusu au kutoyaruhusu,"alisema Kova
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Huseta, Dagan
Kimbwereza, alisema Muingereza huyo (jina linahifadhiwa) amekuwa akitumia
mitandao ya kijamii, kuwashfu Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mzengo
Pinda.
Mwenyekiti huyo
alibainisha kuwa raia huyo wa Uingereza bila ya kuwa na vithibitisho wa kile
anachokisema, amekuwa akikashfu mihimili mingine ikiwamo mahakama,tasnia ya
habari na wananchi kwa jumla.
“Baada ya kufika
ubalozini wawakilishi wawili watawasilisha azimio lenye saini za Watanzania
wakiitaka Serikali ya Uingereza kutoa tamko hadharani kwamba yenyewe haihusiki
wala haisaidii dharau na maovu mengine yanayofanywa na raia wake dhidi ya Taifa
la Tanzania,”alisema Kimbwereza.
Kimbwereza
akionyesha kwa waandishi moja ya chapisho ambalo mtuhumiwa ameandika katika
mitandao ya jamii ni ile inayosema;
Kikwete aitaka
PCCB (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa) kupambana na rushwa hadi katika
Baraza la mawaziri,’kundi moja la majambazi linaliambia kundi jingine la
majambazi kukamata mwizi” .
“Mahakama za Tanzania
zimejaa rushwa na hazina uwezo. Rais ndiye msimamizi wa katiba na yeye ndiye
mhusika mkuu wa ukiukwaji wa sheria” inasomeka moja ya hoja alizoziandika Sarah
katika mitandao ya
kijamii.
Post a Comment