Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors
Patrick Ngowi akisikiliza mawazo ya mmoja wa vijana wajasiriamali mwenye nia ya
kukataka kukuza biashara yake na kuifanya kuwa endelevu wakati wa uzinduzi wa
Mara Foundation ambao uliotoa fursa ya washiriki kuzungumza na wafanyabiashara
waliopiga hatua na wenye uzoefu katika kuendesha biashara zao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Relim Limited Emelda Mwamanga
akimsikiliza mmoja wa washiriki ambaye ni mjasiriamali anayechipukia aliyetaka
kupata uzoefu na mawazo zaidi jinsi ya kuendesha biashara yake.
Mkurugenzi Mkuu wa 361 Degrees ambaye ni Mbunifu
Mkongwe wa Mavazi nchini Tanzania Mustafa Hassanali akimsikiliza mjasiriamali
mdogo mwenye ndoto za kuwa mbunifu wa kimataifa.
Ma-Mentors waliokuja kuzungumza na wafanyabiashara
wadogo kwa ajili ya kuwapa mbinu mbalimbali za kibiashara na kuwaongoza kufikia
malengo yao.
Taasisi ya Mara Foundation ilianzishwa na Ashish
Thakkar ambaye ndie mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Mara Group.
Ashish alitumia muda wake mwingi katika kutimiza
malengo ya Taasisi hiyo kwa kuwa alikuwa na imani na wajasiriamali na kuendeleza
biashara ndogo.
Tangu mwaka 2009 Taasisi hiyo ililenga mtazamo wake na
imefanya vizuri sana nchini Uganda, Tanzania, Kenya na Nigeria katika muelekeo
huo.
Kuanzia mwaka 2013 mikakati ya taasisi ya Mara
Foundation inaendelea kukua katika nchi za Kusini mwa Jangwa la sahara huku
ikiendelea kuongeza wigo wake katika nchi nyingine duniani.
Mara Foundation inafanya kazi ya kubuni na kukuza
uchumi endelevu na kufungua fursa endelevu kwa vijana wamiliki wa biashara za
kati kwa kupitia vituo vya uwezeshaji vya Mara Launchpad na Mara Launch
Fund.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa taasisi ya kibiashara ya
Mara Foundation Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mh.
Dkt. Mary Nagu akizungumza wakati kuzindua taasisi ya Mara Foundation ambapo
amewataka vijana wajasiriamali kutumia fursa ya taasisi hiyo kujijenga
kibiasharaTaasisi ya Mara Foundation yenye makao yake makuu jijini Dubai sasa
imejikita katika nchi za Afrika ambazo ni Uganda, Tanzania, Kenya na Nigenia kwa
lengo kuwasaidia wajasiriamali wadogo kuwezeshwa kimuongozo na kuwa
wafanyabiashara wakubwa ambao wataweza kutoa ajira kwa watu
wengine.
Washiriki na wageni waalikwa wakifurahi jambo wakati
mgeni rasmi Dkt. Mary Nagu akitoa risala kwenye uzinduzi wa Taasisi ya Mara
uliofanyika hivi karibuni kwenye jengo la Mayfair Plaza.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa taasisi ya kibiashara ya
Mara Foundation Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mh.
Dkt. Mary Nagu akikata utepe kuzindua rasmi taasisi hiyo yenye matawi 28 barani
Afrika. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Mara Foundation Nina Werner.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Wageni waalikwa wakishangilia kwa makofi.
MC wa uzinduzi huo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya Problem Solved Eric Mutta akimkabidhisha Mjasiriamali mdogo Peter
Christopher kwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors Patrick Ngowi
(katikati) atakayekuwa mshauri wake wa kibiashara kwa muda wa miezi sita
ijayo.
Mkurugenzi Mkuu wa 361 Degrees ambaye ni Mbunifu
Mkongwe wa Mavazi nchini Tanzania Mustafa Hassanali (katikati) akimpokea mmoja
wa wajasiriamali waliohudhuria uzinduzi wa Mara Foundation kwa lengo la
kuhakikisha anatimiza malengo yake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Relim Limited Emelda Mwamanga
(kushoto) akipata picha ya ukumbusho na kijana aliyemchagua kumsaidia kimawazo
na kumwongoza kwa muda wa miezi sita ijayo mpaka kufikia lengo
lake.
Baadhi ya wageni waliohudhuria uzinduzi wa Mara
Foundation uliofanyika hivi karibuni Mayfair Plaza.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors
Patrick Ngowi (kushoto) na Mkurugenzi Mshirika wa IMMMA Advocates Lawrence Masha
wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mara
Foundation.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Helvetic Solar Contractors
Patrick Ngowi (kushoto) Mkurugenzi Mshirika wa IMMMA Advocates Lawrence Masha
(kulia) na Mkurugenzi wa man Magazine Dismas Massawe (katikati) katika picha ya
pamoja baada ya uzinduzi wa Mara Foundation.
Post a Comment