Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MCHEKESHAJI
maarufu na mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Emmanuel Mgaya, Masanja
Mkandamizaji, amesema kuwa amejipanga imara kuhakikisha kuwa anafanya vitu vya
aina yake katika onyesho la Tumaini Jipya, linalotarajiwa kufanyika mkoani
Morogoro Machi 31, katika Uwanja wa Jamhuri na kushirikisha pia wakali
mbalimbali.
Masanja
Mkandamizaji
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Masanja alisema kuwa amejiandaa vyema kutangaza neon la
Mungu kwa kupitia kipaji chake cha uimbaji wa muziki wa Injili, akiamini kuwa
afya yake itakuwa njema na kuimba pamoja na wadau wao katika onyesho hilo la
Tumaini Jipya.
Masanja
Mkandamizaji
Alisema
ingawa anatamba sana katika ulingo wa uchekeshaji kwa kuwa na aina ya
uzungumzaji na kufurahisha watu wengi, lakini makali yake hayaelezeki katika
uimbaji wa muziki wa injili.
“Nipo
sawa kiafya na naamini Mungu atanibariki kila zuri kwa ajili ya kuimba pamoja
kwenye tamasha hilo la Tumaini Jipya nikiwa na waimbaji wengine wenye makali ya
aina yake.
“Itakuwa
ni siku nzuri kwa siku ya Jumapili ya Machi 31 katika uwanja huo wa Jamhuri,
hivyo naamini watu watakuja kwa wingi kulishuhudia neno likipenya masikioni
mwao,” alisema Masanja Mkandamizaji.
Mbali
na Masanja, wengine watakaofanya onyesho hilo ni pamoja na Martha Mwaipaja,
Stara Thomas, Bahati Bukuku, Sifa John, Joseph Nyuki pamoja na vikundi
mbalimbali vya kwaya vikitajwa kuwapo kwenye tamasha hilo la Tumaini Jipya
litakaloanzia mkoani Morogoro.
Post a Comment