Na Deodatus
Balile, Dar es Salaam
Makubaliano ya pande mbili ya ujenzi wa miundombinu utakaogharimu shilingi trilioni 1.28 (Dola milioni 800) yaliyotiwa saini wiki hii kati ya Dar es Salaam na Beijing yataongeza kukua kwa uchumi wa Tanzania, viongozi wa Tanzania walisema.
Makubaliano ya pande mbili ya ujenzi wa miundombinu utakaogharimu shilingi trilioni 1.28 (Dola milioni 800) yaliyotiwa saini wiki hii kati ya Dar es Salaam na Beijing yataongeza kukua kwa uchumi wa Tanzania, viongozi wa Tanzania walisema.
Rais wa China Xi
Jinping akisalimiana na watu wakati yeye na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
(kulia) wakitembea kwenye zuria jekundu wakati wa kuwasili kwa Xi katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam tarehe 24 Machi.
[AFP/John Lukuwi]
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na Rais wa
China Xi Jinping walisaini mikataba 16 kwa ajili ya miradi ya maendeleo Tanzania
Bara na mikataba mitatu kwa Zanzibar wakati wa ziara ya kiserikali ya Xi Dar es
Salaam tarehe 24 na 25 Machi.
Makubaliano yalifungua njia kwa China
kugharimia na kujenga bandari yenye thamani ya shilingi trilioni 16 (Dola
bilioni 10) huko Bagamoyo na miradi mingine ya miundombinu.
"Ziara ya Rais Xi ni ya kihistoria," Waziri wa
mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Bernard Membe aliiambia
Sabahi. "Licha ya kuweka wazi sera ya China kwa Afrika kupitia Tanzania,
Tanzania imetia saini na China mikataba 19 ya thamani. Mkataba kama huo wa
bandari ya Bagamoyo [mradi] ni uwekezaji wa muda mrefu."
Ikiwa imepangwa kumalizika ifikapo 2017,
bandari ya Bagamoyo -- kaskazini mashariki mwa Dar es Salaam -- itakuwa na uwezo
wa kushughulikia mizigo mara ishirini zaidi kuliko bandari katika mji mkuu wa
Tanzania, ambayo ni bandari kubwa kuliko zote nchini.
"Bandari hiyo [huko Bagamoyo] itakuwa ya
viwango vya juu. Tunajenga bandari ya kizazi cha nne," alisema Balozi wa China
nchini Tanzania Philip Marmo. "Itashughulikia makontena milioni 20 kwa mwaka,
ukilinganisha na [bandari] ya Dar es Salaam, ambayo inashughulikia makontena
800,000 tu kwa mwaka."
Post a Comment