Baada ya siku ndefu ya watu
kupiga kura nchini Kenya, wengi wana hamu kujua rasmi mshindi wa
uchaguzi wa urais. Hata hivyo matokeo ya mwanzo yameanza kutolewa na
tume ya uchaguzi na mipaka Kenya, IEBC.
Matokeo hayo yanaonyesha Uhuru Kenyatta anaongoza kwa asilimia hamsini na nne huku mpinzani wake Raila Odinga akiwa na asilimia arobaini na moja.
13:05 Abdulkarim Taraja akiwa Mt Elgon, anasema kwenye Bofya facebook kuwa anafurahi ambavyo wanaoshindwa wanakubali matokeo ya kura katika eneo hilo
12:59 Blessed Kuriah anasema kwenye ukurasa wa f Bofya acebook, Bofya bbcswahili, kuwa hali ni tulivu katika eneo bunge la Gatundu Mkoa wa Kati
12:57 Uhuru Kenyatta 2,484,760 Raila Odinga 1,884,152
12:46 Mwandishi wetu Jamuhuri Mwavyombo akiwa mjini Mombasa anasema mji umetulia, maduka mengi yangali yamefungwa watu wakiwa na wasiwasi kuangalia hali itakavyokuwa
12:37 Uhuru Kenyatta 2,459,133 Raila Odinga 1,851, 671
12:24 Idadi ya kura kwa wagombea wakuu wa urais Uhuru Kenyatta 2,429,895 Raila Odinga 1,823,384
12:21 Mwandishi wa BBC Ng'endo Angela ambaye yuko katike eneo bunge la Othaya, Mkoa wa kati, shughuli ya kuhesabu kura inarejelewa upya, baada ya mmoja wa wagombea kutaka hilo lifanyike kufuatia madai ya wizi wa kura. Eneo hilo lina ushindani mkubwa ikizingatiwa lilikuwa eneo bunge la Rais anayestaafu Mwai Kibaki na alikuwa amependekeza mmoja wa wagombea kupigiwa kura na watu wa eneo hilo
Post a Comment