Faida ya kampuni kubwa kutokuwa
na kitengo cha kushughulikia masuala ya kampuni kwenye mitandao ya kijamii, ama
kuwa na kitengo kilichodorora, matokeo yake ni kama kwa mfano ambapo mtu mmoja
ameona ajinyakulie ushujaa koko kwa kutumia jina la kampuni ya Shirika la Umeme
Tanzania, TANESCO na kuunda akaunti kwenye tovuti ya Twitter na kujipachika kazi
ya kujibu maswali ya wenye kero na dukuduku zao, vile vile kutoa kauli kana
kwamba ni agizo rasmi kutoka TANESCO.
Wapo watu kadhaa, wakiwemo viongozi na watu wanaoheshimika/aminika katika jamii, wameingia mkenge kwa kuamini kuwa wanawasiliana na TANESCOtz bila kujua hii ni akaunti ya TANESCO_ iliyo feki.
Na kwa kuwa Twitter haijaitambulisha TANESCOtz kuwa akaunti rasmi ya kampuni/public figure (verified official account), hilo limekuwa jambo rahisi kuwapoteza watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwasiliana na wahusika.
Akaunti ya TANESCOtz ilianza ku-tweet tarehe 16 Januari 2011 na tweet yake ya mwisho ni Juni 6 ya mwaka uo huo ikiwa na jumla ya tweets 17 tu wakati akaunti ya TANESCO_ imeanza ku-tweet tarehe 28 ya Februari ya mwaka huu hadi tarehe ya pili ya mwezi Machi 2013 ilikuwa tayari na tweets 169.
Bofya screen-shot moja moja zilizopachikwa hapo ujisomee tweets za TANESCO_

Tweets za TANESCO_ hadi sasa TANESCOtz hawajatamka hadharani
kukubali au kukanusha kuhusika na akaunti hiyo. Pengine TANESCO inaamini kuwa
wananchi wote wana uwezo wa kutambua kuwa hii siyo akaunti yao. Kutokana na kero
za kukatika kwa umeme mara kwa mara na majibu ya TANESCO yasiyoendana na hali
halisi majumbani na kazini, wapo watakaoamini TANESCO_ ndiyo akaunti rasmi ya
TANESCO na majibu hayo ndiyo majibu yao.
Hivi inafahamika kuwa mtu anaweza kukuburuta mahakamani binafsi au kampuni, kwa kutokukanusha au kukubali maneno yanayotamkwa kwa jina lako?
Naam, wapo watu hupeleka kesi mahakamani kushitaki, si kwa lengo la kupata sifa au fidia, bali kushinikiza na kushurutisha mtu au kampuni kutoa funzo kukubali au kukanusha maneno yanayosemwa juu yake, ili kuweka rekodi sahihi kwa jamii kwa lengo la kuwasaidia wanajamii wasibebe dhana potofu kanakwamba ni kweli na kupoteza kumbukumbu sahihi.

*Imeandikwa na Subi-Wavuti
Post a Comment