Mbunge wa jimbo la
Morogoro Kusini Innocent Kalogeries kushoto akimwangalia msaidizi wake, Hamidu
Saidi wakati akiwasha jenereta za kuvuta maji 20 ambazo ofisi yake zimewakopesha
vikundi 12 vya uzalishaji wa chakula na bustani katika jimbo hilo yenye thamani
ya sh 9Milioni katika kijiji cha Sesenga kata ya Mngazi ambavyo vikundi
vyaUmoja, Kazi Kwanza, Twidie vilinufaika na mpango huo.
Hapa akizungumza na
wanavikundi vya Umoja, Kazi Kwanza, Twidie kata ya Mngazi.
Baadhi ya wanavikundi
vya ujasiliamali vya uzalishaji mazao ya chakula na bustani wakiwa wamebeba
mashine hizo baada ya kukopeshwa na ofisi ya mbunge wa jimbo hilo Innocent
Kalogeries.
Mwanavikundi wa kikundi
cha Wazee Mvuha akiwangilia maji katika kitalu kilichopandwa mbegu za
mchicha ambapo kazi hiyo itakuwa imepungua kutokana na kupata mashine za kuvuta
maji kwa ajili ya shughuli za kilimo, mazao ya chakula na
bustani
Mmoja wa mwanakikundi
cha Wazee akiwa mabeba keni yenye maji mara baada ya kuchota maji katika mto
Mvuha ambapo kazi hiyo itakuwa imerahishishwa baada ya kupata mashine ya kuvuta
maji.
Mbunge huyo akizungumza
jambo na wanavikundi vinne vya Muungano wa Wazee wa Mvuha, Tulo Tushikamane,
Tujikwamue na Tushirikiane Kongwa vyote kutoka kata ya Mvuha.
Mwenyekiti wa CCM wilaya
ya Morogoro Vijijini Salum Jazzaa akifafanua jambo juu ya ilani ya uchaguzi ya
mwaka 2010 huku Mbunge wa jimbo hilo Innocent Kalogeries anayenong'oneza na
Mwenyekiti wa kijiji cha Mtamba Paul Mtamani na kulia ni Diwani wa Kisemu Hamza
Mfaume.
Mwenyekiti wa CCM wilaya
ya Morogoro Vijijini Salum Jazza akimkabidhi mmoja wa wanavikundi katika kata ya
Mngazi huku mbunge wa jimbo Innocent Kalogeries kulia akishuhudia kijiji cha
Sesenga.
Na Juma Mtanda,
Morogoro.
MBUNGE wa jimbo la
Morogoro Kusini, Innocent Kalogeries amewataka wanachama wa vikundi vya
wajaliamali kuongeza juhudi za uzalishaji mazao ya chakula na bustani baada ya
mfuko wa jimbo hilo kutoa mkopo wa mashine 20 za kuvuta maji zenye thamani ya sh
9milioni katika jimbo hilo mkoani hapa.
Akizungumza na
wanavikundi 242 kwa nyakati tofauti katika jimbo hilo mkoani hapa, Kalogeries
alisema kuwa jumla ya vikundi 12 vimepatiwa mkopo wa mashine 20 za kuvuta maji
kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na bustani lengo likiwa kuendeleza
juhudi za mkoa wa Morogoro kuwa ghala la chakula.
Kalogeries alisema kuwa
lengo la kutoa mkopo huo kwa vikundi hivyo ni mwendelezo wa ahadi ya utekelezaji
wa ilani ya ccm wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ya kuwawezesha
wananchi katika harakati za kuwakwamua katika dimbwi la umasikini na kufanya
mkoa wa Morogoro unakuwa ghala la chakula.
“Mfuko wa jimbo la
Morogoro kusini umetumia kiasi cha sh 9milioni kwa ajili ya ununuzi wa mashine
20 za kuvuta maji ambapo sasa mutakuwa na uwezo wa kulima mazao ya chakula na
bustani mwaka mzima lakini mashine hizi zitunze ikiwemo na kulipa kiasi cha
marejeshi ya sh45,000 baada ya miezi sita ili na vikundi vingine viweze
kukopeshwa”. Alisema Kalogeries.
Vikundi vilivyofaidika
na mkopo huo wa mashine za kuvuta maji ni pamoja na Muungano wa Wazee wa Mvuha,
Tulo Tushikamane, Tujikwamue na Tushirikiane Kongwa vyote kutoka kata ya Mvuha,
Tushirikiane Group kutoka kata ya Bwakila Chini na Polepole Tugendege kata ya
Bwakila Juu.
Alivitaja vikundi
vingine kuwa ni Jitihada Ufike Vegetable Group kata ya Kinole, Umoja, Kazi
Kwanza, Twidie kutoka kata ya Mngazi, Mshikamano, Kiwamamo vya kata ya Kisaki
vyote vikiwa na jumla ya wananchama 242 kutoka katika vikundi 12 katika tarafa
ya Matombo, Mvuha na Kisaki katika halmashauri hiyo ya wilaya ya
Morogoro.
Kalogeries alisema kuwa
baada ya mfuko huo wa jimbo kutumia kiasi hicho cha sh 9milioni kwa vikundi vya
mazao ya chakula na bustani kazi iliyopo mbele yake ni kuwashawishi vijana
wanaojishughulisha na kutafuta kipato kwa kuendesha pikipiki maarufu (Bodaboda)
kujiunga katika vikundi ili nao wawezeshe kupokopeswa
pikipiki
Post a Comment