……………………………………….
Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha
MAMLAKA
ya mawasiliano Tanzania TCRA,imetangaza kuzima mitambo ya Analojia katika mkoa
wa Arusha na wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro ifikapo ,Machi 31,mwaka huu,
saa 6 usiku na kwamba taratibu zote za kuzima matangazo yote ya televisheni
zimekamilika.
Akizungumza
na vyombo vya habari jijini Arusha,mkurugenzi mkuu wa mawasiliano na
utangazaji,Habbi Gunze alisema kuwa uzimaji wa mitambo hiyo ni mwendelezo wa
zoezi lililoanza rasmi hapa nchini katika jiji la Dar ES Salaa desemba 31 mwaka
2012.
Alisema
katika awamu ya kwanza mikoa mingine ambayo uzimaji wa mitambo ya analojia
umefanyika ni pamoja na Dodoma,Tanga iliyozimwa januari 31,Mwanza,Februari 31
huku mkoa wa Mbeya ukitajiwa kuzimwa Aprili 30 mwaka huu.
Aidha alisema kuwa katika jiji la Arusha tayari ving’amuzi vya matangazo ya televisheni zaidi ya 50,000 zimeshauzwa kwa watu mbalimbali na kufanya mwitikio wa kuhamia dijitali kwa wananchi kukubalika kwa kasi kubwa.
Aidha alisema kuwa katika jiji la Arusha tayari ving’amuzi vya matangazo ya televisheni zaidi ya 50,000 zimeshauzwa kwa watu mbalimbali na kufanya mwitikio wa kuhamia dijitali kwa wananchi kukubalika kwa kasi kubwa.
Alifafanua
kuwa elimu inayotolewa na mamlaka hiyo kupitia vyombo mbalimbali vya habari
inchini imeongeza kasi ya watu kujiunga na digitali na kueleza kuwa watu zaidi
ya asilimia 20% kati ya watu asilimia 24% wanaopata matangazo ya televisheni ya
analojia tayari wamejiunga na mfumo huo.
Haata
hivyo Gunze alisisitiza kuwa mabadiliko hayo katika awamu hii ya kwanza
hayatahusu matangazo kwa njia ya utangazaji wa satelaiti ,waya (cable)na Radio
na kuwataka wananchi wasitupe TV zao za analogia bali watumie ving’amuzi ili
kupata matangazo.
Awali
meneja wa kanda ya kaskazini,Inginia Aneth Matindi alisema kuwa kumekuwepo na
changamoto mbalimbali kwa wanachi juu ya uelewa wa matumizi ya ving’amuzi
,ufahamu wa kuingia digitali pamoja na huduma kwa wateja ,ambapo alisema kuwa
elimu inahitajika ziaidi ili kuondoa changamoto hizo na kuwapa uwelewa
wananchi.
Post a Comment