Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mbunge wa Viti maalum Chadema (Kwimba) Mh Leticia Nyerere Atembelea atembelea ofisi za bunge la Marekani mjini Washington DC

 

 Mbunge wa Viti maalum Chadema (Kwimba) Mh Leticia Nyerere akisalimiana na Mtaalamu wa kamati ya Bunge la Marekani anayeshughulikia Mambo ya Nje Tamara Klajn.
 Mbunge wa Viti maalum Chadema (Kwimba) Mh Leticia Nyerere akijadili mambo mbalimbali na Mtaalamu wa kamati ya Bunge la Marekani anayeshughulikia Mambo ya Nje Tamara Klajn.
*****
Mbunge wa Viti maalum Chadema (Kwimba) Mh Leticia Nyerere amefanya ziara ya kutembelea Ofisi za Bunge la Marekani mjini Washington DC Ijumaa 15 Machi 2013. Lengo la ziara hiyo ya Mh Leticia Nyerere ni kutaka kujua namna Mabunge mawili ya Marekani yanavyofanya kazi. Bunge la Marekani limegawanyika katika sehemu kuu mbili yaani Bunge la wawakilishi (House of Representative) na Bunge la Seneti (Senate). Katika ziara hiyo Mh Leticia Nyerere alipokelewa na Mtaalamu wa kamati ya Bunge la Marekani anayeshughulikia Mambo ya Nje Tamara Klajn.
 
 Ikumbukwe katika Mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba Spika wa Bunge la Tanzania Mh Anna Makinda alitoa maoni kwa kushauri katika Tume ya Katiba tuwe na Mfumo wa Mabunge mawili yaani Bunge la wawakilishi na Bunge la seneti ili kuboresha mfumo wa Uendeshaji wa Bunge la Tanzania.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top