Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo ACP, Charles Kenyela
---
Jeshi
la Polisi mkoani Dar es Salaam kanda ya Kinondoni limekataza maandamano
yaliyokuwa yamepangwa kufanyika tarehe 16 Machi 2013 yaliyokuwa
yameiratibiwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika yaliyolenga kufika katika
Wizara ya Maji ili kufikisha ujumbe kwa Waziri wa Maji, Prof Maghembe
kuhusu kero ya maji katika jimbo hilo ambayo haijatatuliwa wala kupatiwa
ufumbuzi kwa muda mrefu. Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo ACP, Charles
Kenyela amesema endapo maandamano hayo yatafanyika:
1. Upo wasiwasi wa kutokea kwa vurugu pale watakaposhindwa kufikia muafaka kuhusu hoja zao.
2. Amewasiliana na Ofisi ya Waziri husika na kufahamishwa kuwa haina taarifa rasmi za ujio wa maandamano hayo.
3. Barabara yatakakopita maandamano hayo ipo katika ujenzi na hivyo maandamano hayo yatazuia shughuli za mkandarasi kukamilisha kazi yake kwa wakati na kuisababishia Serikali hasara.
Credits: Lukaza Blog
Post a Comment