Wadau mbalimbali wakishiriki semina Kuhusiana na mfuko wa afya ya jamii CHF Wilayani RUANGWA |
Mkuu wa wilaya pamoja na Meneja wa Nhif Lindi wakitandika
moja ya shuka zilizokabidhiwa |
MKUU wa wilaya Ruangwa mkoani Lindi Agnes Hokororo amemtaka mganga mkuu wa wilaya hiyo kuzitumia fedha za mfuko wa afya ya jamii kununulia dawa na vifaa tiba ili kuondoa upungufu wa madawa
unazozikabili zahanati na vituo vya afya mara kwa mara katika wilaya hiyo.
Wito huo ameutoa wakati alipokuwa anafungua mafunzo ya elimu ya kata kwa kata kwa wadau na wanachama wa mfumo wa taifa bima ya afya na jamii uliofanyika wilaya ruangwa jana. hokororo alisema kuwa kero nyingi zinatolewa na jamii kuhusiana na huduma za mbovu zinazotolewa kwenye baadhi ya vituo vya afya, zahanati, inasababishwa na watendaji wasio waadilifu katika sekta ya afya kwa ukosefu wa dawa wilayani humo.
Alisema wapo watumishi wachache wenye malengo ya kuvipaka matope vituo vya kutolea huduma kwa sababu zao binafsi na imani potofu kuwa wanachama wa mfuko wa bima ya afya ni wagonjwa wanaopata huduma bure.
Aidha alifafanua kua ni wajibu wa watoa huduma wa sekta ya afya kuwa wabunifu na kuzingatia wajibu wao, maadili na kufuata masharti yaliyowekwa na serikali ili waendelee kujijengea heshima na kulinda heshima za sekta ya afya.
Post a Comment