Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ametoa salamu za pongezi kwa Papa Mpya wa
Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis I kwa kuchaguliwa kuliongoza Kanisa hilo
Duniani.
Lowassa ametuma salamu
hizo kwa Papa kupitia ukurasa wake wa Facebook na pia ametoa pongezi kwa
Wakatoliki wote Duniani kwa kumpata Kiongozi huyo ambaye kiasili na jina lake ni
Mt. Francis ni mtu wa kawaida.
Huu ndio ujumbe Kamili
aliyouandika Ndugu, Edward Lowassa katika Ukurasa wake
huo:-
“Hongera Cardinal Jorge Mario Bergoglio kwa kuchaguliwa kuwa
Pope Francis I,
Na pia hongera wakatoliki wote duniani zaidi ya bilion 1 kwa kumpata Kiongozi ambaye kiasili na jina alilolichagua la Mt Francis ni mtu aliyeishi maisha ya kawaida na ya kuwapenda masikini katika maisha yake yote ya uitumishi.
Naamini sasa dunia mpya ya watu masikini kupata tumaini la maisha imezaliwa, na kwa pamoja tuungane kumpongeza na kumtakia mafanikio mema kiongozi wetu mkuu wa Kanisa katoliki duniani.
Na pia Roho mtakatifu amwongoze katika kuzikabili changamoto za kanisa duniani kote.” Alimalizia Lowassa katika Ujumbe huo.
Credits: Father Kidevu Blog
Post a Comment