Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MHARIRI MKUU MTENDAJI WA KAMPUNI YA NEW HABARI (2006) AZIDI KUIMARIKA ... MTAZAME ALIVYO SASA HOSPITALINI

 



Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu na Mhariri Mtenaji wa Free Media, Ansbert Ngurumo wakiwa na Mhariri Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) na Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri, Absalom Kibanda nchini Afrika Kusini.






Taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Jukwaa la wahariri Neville Meena aliyeko Afrika Kusini katika Hospitali ya Mirlpak anakopata matibabu Kibanda



Wapendwa Wahariri,

Tupo katika hosiptali ya Milpark, Johannesburg nchini Afrika Kusini kumjulia hali Mwenyekiti wetu, Absalom Kibanda ambaye kama mnavyofahamu anapatiwa matibabu kutokana na tukio la kushambuliwa kwake.



Pamoja nami, pia wapo Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu na Mhariri Mtenaji wa Free Media, Ansbert Ngurumo.



Jana (Ijumaa) kutwa tulishinda naye hosipitalini na kwa ujumla hali yake inaendelea kuimarika vizuri. Kama tulivyowaarifu tangu juzi, ameanza mazoezi mepesi ya kusimama na kutembea na anaweza kukaa kwa muda na kushiriki mazungumzo. Kwa hakika amechangamka na anatia moyo.



Hata hivyo, bado mwenyekiti wetu ataendelea kubakia hosipitalini kwa matibabu zaidi kama wanavyoshauri madaktari wake. Jambo la msingi tuendelee kumwombea katika sala zetu na wale ambao watapata fursa wafike kumjulia hali na kumtia moyo.



Kwa muda tutakaokuwa hapa tutaendelea kuwajulisha maendeleo ya afya yake. Pokeeni pia picha ambazo tumepiga tukiwa pamoja naye hosipitalini akiwa ameketi kwenye kiti.
 
Credits: AmaniTanzania
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top