Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MVUA ZAKATA MAWASILIANO KATI YA KARATU NA MONDULI


 




MVUA zinazondelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini zimeasbabisha
kukatika kwa mawasiliano ya barabara kati ya wilaya za monduli na karatu
mkoani arusha baada ya daraja la mMto Kirurumo linaounganisha wilaya hizo
kufunikwa na mawe na kusababisha maji kukata sehemu kubwa ya barabara hiyo
Mvua hizo zinazodaiwa kuanza kunyesha kuanzia saa tisa usiku pia
zimesababisha idadi kubwa ya nyumba katika bonde la mto wa mbu kujaa
maji

waandishi wa habari wameshuhudia asilimia kubwa ya wasafiri wakiwemo
watalii waliokuwa safarini wakiwa wamekwama katika eneo hilo na wengine
wakijaribu kutembea kwa miguu kutafuta namna ya kuunganisha safari bila
mafanikio .
Kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo aliyetembelea
eneo hilo na kujionea hali halisi pamoja na kuelezea hatua zinazochukuwa
na serikali kukabiliana na tatizo hilo amevitaka vyombo vinavyohusika
kutoa vibali vya muda kwa magari ya abiria kutumia njia zingine wakati
matengenezo ya eneo hilo yakiendelea
Bw Mulongo ametaja barabara zinazohitarajiwa kutumika kwa dharura wakati
daraja hilo linashughulikiwa kuwa ni pamoja wasafiri wanaokwenda mwanza,
Musomaa kutumia barabara ya babati kupitia Singida na wanaoenda loliondo
kutumia barabara ya Engaruka
Kwa upande wa wasafiri wanaokwenda karatu wameshauriwa kutumia barabara
inayopitia Bababti , mbulu hadi karatu
Katika hatua nyingine Bw Mulongo amewataka wananchi wanaoishi ndani ya
bonde la mto wa mbu kutii agizo la serikali la kuondoka katika eneo
hilo na kuhamia kwenye maeneo waliyokwisha pangiwa kama hatua ya kuepusha
madhara zaidi
Amesema wananchi hao walishapewa maeneo mengine lakini wamekuwa wagumu
kuhamia hivyo ni vyema wakaona umuhimu wa kuondoka eneo hilo kabla madhara
hayajawa makubwa zaidi
Kwa upande wake meneja wa wakala wa barabara mkoa Arusha Bw Deusi Kakoko
amesema kazi ya kufungua barabara hiyo inaendelea licha ya kuwa inaweza
kuchukuwa zaidi ya siku mbili na kwamba hasara iliosababishwa na mvua
hizo inaweza kufikia zaidi ya milioni 400
Bw Kakoko amefafanua kuwa zaidi ya mita mia mbili za barabara zimekakatika
na kwamba kinachofanyika sasa ni hatua za dharura tu na baada ya hapo
watafanya tahimini upya ya namna ya kudhibii eneo hilo
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameiomba serikali kutaafuta ufumbuzi wa
kudumu wa tatizo hilo kwani licha ya kuwa limekuwa kero ya kudumu
limekuwa likiisababishia serikali hasara ya kujenga daraja kila mwaka .
Slource :Maelezo
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top