Mwili wa Marehemu Hugo Chavez katika gari. |
Maelfu ya raia wa Venezuela wakiusindikiza mwili wa aliyekuwa rais wao. |
Mwili wa Chavez umelazwa katika kituo cha mafunzo ya kijeshi mjini Caracas na marais wa nchi jirani walifika kutoa heshima zao za mwisho akiwemo Rais wa Bolivia |
Mwili wa mareheu rais Hugo
Chavez wa Venezuela, umelazwa katika kituo cha mafunzo ya jeshi katika mji mkuu
Caracas Mapema leo mwili wa marehemu Chavez ulipitishwa kwenye umati mkubwa wa
wafuasi wake katika mitaa ya mji mkuu Caracas.
Watu wengi waliangua
kilio huku wakichukua picha za kiongozi wao aliyefariki dunia . Mama yake na
watoto wake walikusanyika mbele ya jeneza kutoa heshma zao. Makamu wa rais
Nicolas Maduro anaongoza shughuli hiyo. Mwili wa rais Chavez umepelekwa katika
chuo cha kitaifa cha mafunzo ya kijeshi ambapo utazikwa kesho
Ijumaa.
Bwana Chavez alifariki
akiwa umri wa miaka 58 baada ya kuugua Saratani kwa zaidi ya miaka miwili.
Maelfu ya watu awali walikwenda barabarani mjini Caracas kutoa heshima zao za
mwisho kwa Chavez wakifuatana na gari lililokuwa limebeba jeneza lake kuelekea
katika chuo cha mafuzno ya jeshi.
Mazishi ya kitaifa ya
Chavez yatafanyika Ijumaa. Mkuu wa ulinzi wa Rais alinukuliwa akisema kuwa
alikuwa na bwana Chavez alipofariki. Generali Jose Ornella, alisema kuwa Chavez
alifariki kutokana na mshtuko wa moyo na katika siku zake za mwisho kabla ya
kifo cha ealisema angependa kuendelea kuishi.
Jeneza lake lililokuwa
limefunikwa bendera ya nchi hiyo uliwekwa katika ukumbi ambao ni kumbukumbu ya
waliopigania uhuru wa watu wa Amerika ya Kusini.
Maelfu ya watu walipanga
foleni kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Chavez, wakiwemo maafisa wa
serikali na viongozi wa Amerika ya Kusini,kama Rais wa Bolivia Evo Morales na
Rais wa Argentina Cristina Fernandez de
Kirchner.
Post a Comment