Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepunguza vikwazo vya silaha kwa Somalia, ambapo nchi hiyo sasa itaruhusiwa kununua silaha ndogo ndogo na baadhi ya vifaa vya kijeshi.
Baraza hilo limekubaliana kupunguza vikwazo hivyo kwa mwaka mmoja.
Vikwazo hivyo viliwekwa tangu mwaka 1992 baada ya wababe wa kivita kuanza vita vilivyodumu muda mrefu.
Hatua hiyo imechukuliwa kwa ajili ya kuvisaidia vikosi vya Somalia kujimarisha na kugawa mamlaka ya serikali kwenye maeneo ambayo hivi karibuni yamekuwa yakidhibitiwa na wapiganaji wenye itikadi kali za Kiislamu.
Post a Comment