Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akizindua kijitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi
za Tume ya Haki ya Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam.
Kitabu hicho kimeandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,
Ubalozi wa Uingereza Nchini na Taasisi ya Jumuia ya Madola
inayoshughulikia haki za binadamu. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Tume
hiyo Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Manento akifuatiwa na Katibu Mtendaji
wa Tume Mary Massay.
Naibu
Balozi wa Uingereza nchini Julian Chandler akielezea jinsi nchi yake
ilivyoona umuhimu wa kuandaa kitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu
kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza wakati wa uzinduzi wa kitabu
hicho uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi
za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akifuatiwa
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Manento.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Jumuia ya Madola inayoshughulikia haki za binadamu Sarah
Mount akielezea umuhimu wa kitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu
kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza wakati wa uzinduzi wa kitabu
hicho uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishna wa Tume hiyo Bernadeta Gambishi.
Wadau mbalimbali wa haki za binadamu na utawala bora wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa kitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi
za Tume ya Haki ya Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam.
Kitabu hicho kimeandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,
Ubalozi wa Uingereza Nchini na Taasisiya ya Jumuia ya Madola
inayoshughulikia haki za binadamu. Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Post a Comment