Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS KIKWETE ASHIRIKI HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA KIGURUNYEMBE, MOROGORO

 




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013 akiongozana na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude tayari kuhudhuria harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe. Zaidi ya Shilingi milioni 250 zilipatikana katika harambee hiyo, ikiwa ni zaidi ya lengo la kupata milioni 200 walilojiwekea.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili akimkabidhi mjumuisho wa michango Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisimamia harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013. Kuume kwake ni Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi kwa watawa keki maalumu iliyopigwa mnada na kununuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni moja. Aliitoa keki hiyo kama zawadi kwa watoto yatima wanaolelewa na watawa hao.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude wakipokea keki maalumu iliyopigwa mnada na kununuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni moja.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwakaribisha wachangiaji wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude wakiongea wakati wa harambee hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha mmoja wa wachangiaji kupiga naye picha na kuchanga shilingi milioni moja wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.
Sehemu ya waliohudhuria harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na kamati ya harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013. PICHA NA IKULU.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top