Ndugu zangu,
Uchoyo ni hulka ya mtu. Uchoyo si jambo jema. Na mchoyo akizidisha uchoyo wake mwisho hata yeye mwenyewe hulala na njaa.
Maana,itatokea nyumbani kwake atafika mgeni aliyeshiba. Mchoyo ataona tabu kupika chakula na mgeni naye ale. Anaweza kuhangaika na vikombe vya chai akisubiri mgeni wake aondoke.

Usiku mwingi utaingia, mgeni ataomba alale kwa mwenyeji wake. Mchoyo ataona aibu kumnyima hifadhi mgeni wake.
Lakini, kwa vile ana hulka ya uchoyo, na anaona tabu kupika chakula na mgeni wake naye ale, basi, mchoyo naye anaweza kulalia kikombe cha chai huku mgeni wake akiwa amelala na shibe!
Ni Neno La Usiku Huu. ( Pichani ni chai yangu ya usiku huu, HAIHUSIANI na Neno hili!)
Maggid,
Msamvu.
Post a Comment